MVIWATA YAITAKA SERIKALI KUTOA ELIMU KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUEPUSHA MIGOGORO.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa mtandao wa wakulima Kilimanjaro(MVIWATA)Bakari Mbaga akitoa taarifa yake kwenye mkutano mkuu wa sita wa mtandao huo,uliofanyika kwenye hotel ya moshi view. |
Wananchama wa mtandao wa wakulima mkoani Kiliamanjaro(MVIWATA)Wakisikiliza kwa umakini hoja mbalimbali zilizozungumzwa na viongozi wa mtanao huo. |
Wananchama wa mtandao wa wakulima mkoani Kiliamanjaro(MVIWATA)Wakisikiliza kwa umakini hoja mbalimbali zilizozungumzwa na viongozi wa mtanao huo. |
Mmoja wa wanachama akizungumza jambo kwenye mkutano huo. |
Serikali imetakiwa kutoa
elimu kwa wakulima na wafugaji ili kuepusha migogoro ya ardhi ambayo imekuwa
ikitokea mara kwa mara hususani ni katika Wilaya za tambarare zilizopo Mkoani
Kilimanjaro.
Ushauri huo umetolewa na
aliyekuwa mwenyekiti wa Mtandao wa Vikundi vya wakulima wa
Kiliamanjaro(MVIWATA)Bakari Mmbaga wakati wa mkutano mkuu wa sita wa mtandao
huo.
Alisema kuwa kumekuwepo na migogoro ambayo
imekwisha kutokea sehemu mbalimbali nchini na kusababisha maafa makubwa ikiwemo
mapigano na wananchi kupoteza maisha lakini bado Serikali imekuwa ikiendelea
kulifumbia macho suala hilo.
Mbaga alisema kuwa zipo
Wilaya kama ya Same tayari mapigano hayo
yamekwishaanza kutokea kwenye maeneo ya Ruvu kwa wakulima na wafugaji
kuchomeana nyumba na kuumizana hali ambayo alisema kuwa inaendelea kusambaa kwenye Wilaya za
tambarare Wilaya ya Mwanga.
Katika wakati mwingine
alisema kuwa mtandao huo ulifikiri mpango wa Serikali wa kilimo kwanza
ungemkomboa mkulima lakini bado mkulima amekuwa ni mtu wa kutaabika hususani
baada ya kuongezwa kwa masharti kwenye vocha za pembejeo.
“Kipindi cha nyuma masharti
ya vocha yalikuwa nafuu kidogo tofauti na sasa hivi mkulima anatakiwa alipe
shilingi 128,000 ndipo apatiwe vocha sasa huku ni kumsaidia mkulima wa kawaida
au ni kizidi kumkandamiza”Alisema Mmbaga.
Kwa upande wake mratibu wa
mtandao wa mviwata Alex Urio alisema kuwa mkutano huo mkuu ulikuwa ufanyike
mwaka jana lakini ulishindwa kufanyika kutokana na kukabiliwa na uhaba wa
fedha hivyo kulazimika kuufanya mwaka
huu.
Hata hivyo kwenye mkutano
huo mkuu ulifanyika uchaguzi wa viongozi wa mtandao huo wa mviwata
ulifanyika kuwachagua Seraphine Mdee
kuwa mwenyekiti,Zahara Kidaya Makamu Mwenyekiti,Frida Msuya mtunza hazina,huku
wajumbe wakiwa ni philipo Samson,rozin mushi na henry mallya.
No comments:
Post a Comment