Saturday, May 19, 2012

TAMASHA LA NYIMBO ZA KITAMADUNI VS BONGOFLEVA LAFANA NA KUVUTA HAMASA ZA WAKAZI WA MOSHI.

Wamasai wakiwa stagini wakiimba nyimbo zao za asili ya kimasai kwenye tamasha hilo lililokuwa limeandaliwa na Endeleza Foundatio.

Vikundi vya ngoma kutoka tamaduni mbalimbali vilihudhiria tamasha hilo.

Mkuu mpya wa Wilaya ya Moshi Dr Ibrahim Msengi akiwasalimia wananchi waliofika kwenye tamasha hilo ambaye alikuwa mgeni rasmi

Hapa Mkuu huyo wa Wilaya Dr Ibrahimu Msengi akiwa na vikundi vya ngoma mbalimbali za kitamaduni kabla ya kufungua rasmi tamasha hilo.


Mkuu wa Wilaya ya Moshi Ibrahim Msengi akipiga ngoma kama ishara ya kufungua tamasha hilo la kitamaduni vs Bongp Fleva kwenye viwanja vya Mandela Pasua Mjini Moshi.


Wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva waliokuwepo kama wakina Inspekta Haron Babu,Luteni Kalama kutoka gangwe Mobu,

Hapa Inspekta na mwenzake wakifanya mambo kuwapagawisha wananchi na vikundi mbalimbali vya sanaa vilivyofika kwa siku ya leo..
Akiindua tamasha hilo Mkuu wa Wilaya ya Moshi Dr Ibrahim Msengi amesema Moja ya mambo ambayo yanaendelea kuubomoa kama  siyo kutokomeza kabisa  utamaduni wa watanzania ni pamoja na utandawazi ambao umekuwa ukichangia wananchi hususani vijana kushabikia tamaduni za magharibi  kusahau tamaduni za kiafrika.

Mkuu huyo wa Wilaya akizungumza na umati wa wananchi waliohudhuria tamasha hiloambalo limehusisha nyimbo mbalimbali ikiwemo zile za kiasili ambazo zinazounzi utamaduni wa kitanzania na kufanyika kwenye viwanja vya mandela kata ya pasua manispaa ya moshi amesisitiza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa waannchi kuendelea kuuenzi utamaduni wao
Amesema kuwa mahali popote utakapoenda utamaduni hutumika kama kitambulisho kama itakuwa ni lugha fulani au mavazi au chochote kile ambacho kitakuwa kinatambulisha utamaduni wako basi inakuwa ni kitambulisho kwako.
. 
Kwa upande wakeMratibu wa tamasha hilo Ismail Mnikite kutoka endeleza foundation tamasha  ambalo limehudhuriwa na ngoma za makabila mbalimbali amesema kuwa lengo la tamasha hilo ni kuhamasisha, kuendeleza na kuimarisha zaidi utamaduni wetu baada ya kuadhiriwa kwa kiasi kikubwa na utandawazi.


No comments:

Post a Comment