Tuesday, May 8, 2012

 WAANDISHI wa habari washauriwa kuandika Makala.

mhadhiri wa chuo kikuu cha mtakatifu
Augustino Peter Mutaba wakati akitoa semina kwa waandishi wa habari
mkoani Kilimanjaro juu ya uandishi wa makala iliyoandaliwa na muungano
wa vilabu vya uandishi wa habari nchini(UTPC) ambayo leo yameingia siku ya pili.

 Waandishi wa habari mkoani Kilimanjaro wanaohudhuria mafunzo hayo.

 WAANDISHI wa habari washauriwa kuandika habari za Makala  makala na kutokuogopa
gharama na muda kwani makala ni jamvi la habari linaloelezea jambo kwa
kina na linaigusa jamii moja kwa moja.

 Ushauri huo umetolewa na mhadhiri wa chuo kikuu cha mtakatifu
Augustino Peter Mutaba wakati akitoa semina kwa waandishi wa habari
mkoani Kilimanjaro juu ya uandishi wa makala iliyoandaliwa na muungano
wa vilabu vya uandishi wa habari nchini(UTPC)na kuratibiwa na klabu ya
uandishi wa habari mkoani Kilimanjaro(MECKI)

Mutaba alisema baadhi ya waandishi huogopa kuandika makala kutokana na
gharama,muda na kutozingatia utafiti juu ya jambo wanalotaka
kuliandika na kuwatoa hofu kuwa ili makala iweze kuwa nzuri na yenye
kuigusa jamii moja kwa moja inahitaji muda na kuigharamikia.

Aliongeza kuwa,makala kama jamvi ni vyema ikazingatia mambo muhimu
yaliyokusudiwa kuandikwa na ikawalenga jamii moja kwa moja badala ya
kuandika makala inayochochea jambo Fulani ikiwemo vurugu.


Kwa upande wao washiriki wa warsha hiyo ya siku nne waliushukuru umoja
wa vilabu vya waandishi wa habari UTPC kwa kuwaandalia mafunzo hayo
pamoja na klabu ya waandishi wa habari mkoani Kilimanjaro kwa kuomba
na kuratibu mafunzo hayo kutokana na kutoa mwanga kwa washiriki
kufahamu namna ya kuandika makala isiyo ya kichochezi.

No comments:

Post a Comment