KIKUNDI
cha akina mama cha Ndekira kilichopo Kibosho Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani
Kilimanjaro kimekuwa mkombozi kwa mwanamke katika kuwaelimisha kutambua haki zao hususani
mfumo dume,pamoja na kuwasaidia watoto yatima,wanaoishi kwa matumaini na
mazingira magumu kupata elimu na mahitahi muhimu.
Kikundi
cha Ndekira ni moja ya matawi ya kikundi cha akina mama wanaopambana na Ukimwi
Mkoani Kilimanjaro(KIWAKUKI)ambacho kinawaunganisha akina mama wa kata 3 za
Kibosho Mashariki,Kibosho Kati,na Kata ya Kirima.
Hayo
yalibainishwa
Mwenyekiti wa Kikundi hicho Catherina Bendict wakati akizungumza na blog hii ambapo amesema katika kutambua hali
iliyopo kuhusu mahitaji ya vituo vya maarifa na taarifa ya ukombozi
katika
ngazi ya jamii vinavyoundwa na mtandao mwaka huu mikoa mbalimbali hapa
nchini.
Alisema
kuwa kupitia kikundi hicho wakina mama wamekuwa wakipata jukwaa la kudajili
mambo mbalimbali yanayowahusu wanawake,ikiwemo kuwasaidia wanawake wengine
ambao wamekuwa wakizikosa haki zao kutokana na mfumo dume na kunyimwa na
wanaume haki zao ikiwemo kujiunga kwenye vikundi mbalimbali.
Kwa
upande wa watoto yatima na ambao wanaishi kwa matumiani kikundi hicho
kinawapatia mahitaji mbalimbali ambapo mpaka sasa kikundi kina watoto yatima
wanaosomeshwa na kikundi,na kueleza kuwa tangu mwaka 2004 wametumia zaidi ya
million 4 kwa ajili ya mahitaji ya watoto hao.
“Kikundi
kilianzishwa mwaka 2004 na mpaka sasa hatuna miradi ambayo inaweza kutuingizia
kipato kwa ajili ya kuwahudumia watoto hao,tumekuwa tukifanya sherehe na
kualika wageni mbalimbali ambao hutuchangia ambapo kwa sasa ni mradi wa viti
ndio tunategema”Alisema Catherina.
Wakielezea
changamoto zinazowakabili kwenye warsha hiyo,walisema kuwa kikundi hicho
kinakabiliwa na ukosefu wa ofisi kwa sasa ambapo kwa sasa wapo chini ya
hospitaki ya Kibosho,pamoja na ukosefu wa fedha kwa ajili ya kuendeshea kazi za
ofisi.
“Kikundi
chetu kimekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kwa jamii lakini bado
tunahitaji elimu zaidi kwa kujengewa uwezo ili kuweza kuwa mkombozi wa mwanamke
na watoto hususani katika maeneo ya vijijini ambayo mfumo dume bado ni
tatizo”Alisema.
|
No comments:
Post a Comment