WATU WALIOPOTEZA MAISHA KWENYE AJALI YA GARI LA MBUNGE WA ROMBO JOSEPH SELASINI WAONGEZEKA.
Idadi ya Watu waliopoteza maisha kwenye
ajali ya gari alilokuwa akiendesha Mbunge wa Rombo Josephy Selasini
vimeongezeka na kufika watu wanne baada ya watatu kufariki eneo la
tukio huku mmoja akifariki akipatiwa matibabu katika hospitali ya
Rufaa ya KCMC.
Kwa Mujibu wa taarifa kutoka kwa
kamanda wa polisi Mkoani Kilimanjaro Absalom Mwakyoma kwa waandishi
wa habari alisema kuwa ajali hiyo ilitokea may 24 majira ya saa 19:00
katika barabara kuu ya Moshi kuelekea Arusha eneo la Chuo cha Ufundi
Bomango'ombe Wilayani Hai.
Alisema kuwa gari hilo ambalo alikua
akiendesha Mwenye ambalo lilikuwa na nambaza usaji T 441 BRT aina ya
Toyota Land Cruiser lilikuwa na abiria sita na wanne wameweza
kupoteza maisha.
Waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo ni
pamoja na mama yake mzazi wa Joseph Selasini Catheriner Roman
Selasini(80),Agatha Jerome Mahoo mama mkwe wa Selasini,(85)mkazi wa
Rombo ambaye ni mkulima pamoja na wanawake wawili ambao
hawajatambulika majina yao mmoja akikadiriwa kuwa na umri wa miaka
70-75 ambaye inasemekana ni pia ni Shangazin wa Joseph Selasini na
mwingine mwenye ambaye umri wake unakadiriwa kuwa 35-40.
Majeruhi kwenye ajali hiyo ni pamoja na
Mke wa Selasini,Digna Kavishe,(43)ambaye amepata majeraha sehemu za
kichwa na hali yake siyo nzuri,pamoja na Joseph Selasini Mwenyewe
ambaye amepata majeraha kwenye bega pamoja na mkono wa kulia ila hali
yake inaendelea vizuri.
Chanzo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni
mwendokasi pamoja na kupasuka kwa gurudumu la mbele baada ya gari
hilo kuingiliwa na pikipiki mbele na kukosa mwelekeo.
Miili ya Marehemu imehifadhiwa kwenye
hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa ajili ya taratibu za mazishi.
No comments:
Post a Comment