NAIBU WAZIRI WA MAJI GERSON LWENGE AKIBIDHI CHETI CHA UTOAJI HUDUMA KWA VIWANGO VYA KIMATAIFA KWA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAJI TAKA MOSHI(MUWSA). |
MEZA KUU,(kulia)MKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAJI TAKA MUWSA ANTONY KASONTA,(kushoto kwake)MKUU WA WILAYA YA MOSHI MUSA SAMIZI,aliyevaa suti ya kaki NAIBU WAZIRI WA MAJI GERSON LWENGE,ANAFUATIWA NA MWENYEKITI WA BODI YA MAMLAKA HIYO. |
NAIBU WAZIRI WA MAJI GERSON LWENGE AKIONYESHA CHETI CHA
UTOAJI UTOAJI
HUDUMA KWA VIWANGO VYA KIMATAIFA(ISO)KILICHOTOLEWA KWA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAJI TAKA
MJINI MOSHI MKOANI KILIMANJARO.
|
NAIBU WAZIRI WA MAJI GERSON LWENGE AKISOMA HOTUBA YAKE. |
NAIBU WAZIRI WA MAJI GERSON LWENGE AKIKABIDHI VYETI KWA WADAU WA MATUMIA MAJI. |
PICHA YA PAMOJA NA NAIBU WAZIRI,NA VIONGOZI MBALIMBALI.
NAIBU WAZIRI WA MAJI GERSON LWENGE AMEKABIDHI CHETI CHA
UTOAJI UTOAJI
HUDUMA KWA VIWANGO VYA KIMATAIFA(ISO) KWA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAJI TAKA
MJINI MOSHI MKOANI KILIMANJARO.
Akuzungumza kwenye hafla ya
kukabodhi Cheti hicho alizungumzia mafaniko mbalimbali yaliyopatikana kwenye
mamlaka hiyo ikiwemo utendaji,Utaoji wa huduma,ukaguzi wa mahesabu pamoja na
ukusanyaji wa maduhuli.
Alisema kuwa watu wanaopata maji
safi na majitaka kwa Manispaa ya Moshi ni asilimia 97,na wanaopata huduma ya
maji taka ni asilimia 46 kwa wakazi wote wa manispaa hiyo.
Lwenge alisema kuwa suala la
huduma ya maji lipo kwenye mkakati wa kitaifa wa kukuza uchumi na kuondoa
umaskini(MKUKUTA)hivyo mamlaka zote nchini zinapaswa kutoa hudama hiyo na
kuhakikisha zinapata cheti cha utoaji huduma bora kitaifa.
Hata hivyo alisema kuwa mamlaka
zinajitahidi na kuendelea kutoa huduma,ambapo hivi sasa zimefika mamlaka 3
nchini rusha,Tanga na Moshi na kutaka mamlaka nyingine kuiga kwa ambazo
zinafanya vizuri..
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Mamlaka hiyo Anthony Kasonta alisema kuwa tangu kuanza kutunukiwa
cheti hicho katika mamlaka hiyo wameshaboresha mapungufu yaliyokuwepo ikiwemo ununuzi
wa jenereta kwa ajili ya kutumika kuweka dawa ya kutibu maji kwenye vyanzo vya
maji pindi umeme wa Tanesco unapokatika.
Kasonta alisema kuwa yapo mambo
mengi ambayo yana umuhimu wa kuboreshwa lakiniutekelezaji wake unahitaji muda
mrefu,kama kuboresha jingo la huduma kwa wateja,ofisi ya mfumo wa kukusanya
maoni pamoja na mawasiliano kwa wateja na wadau.
No comments:
Post a Comment