Wednesday, May 30, 2012

TANZANIA YAPATIWA MKOPO WA ZAIDI YA MILLION 30 NA BENKI YA BADE.

 waziri wa fedha wa Tanzania Dr,Wiliam Mgimwa akiwa mkurugenzi wa benki ya Badea  Abdelaziz Khelef wakibadilishana mikataba ya mkopo mara baada ya kutia saini
 wakibadilishana mawazo
 waziri wa fedha wakiwa wanaongozana na waandishi kwa ajili ya kuongea nao
 mdada wa libeneke la kaskazini akisalimiana na waziri wa fedha
waziri wiliam mgimwa akiwa anaweka saini ya mkataba wa mkopo wa bilioni 34.5 kutoka katika benki ya maendeleo ya afrika tok nchini uharabuni (BADEA)
waziri wa fedha zazibar Yusuphy mzee akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya mkopo huo kutolewa

Mwandishi wa habari wa gazeti la majira Pamela Mollel akiwa anabadilishana mawazo na  Tiganya
Habari na Libeneneke la Kaskazini.

 

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Dodoma, Bi. Moza Said (katikati), akiangalia maji yaliyochanganywa na udongo wenye dhahabu kwenye machimbo mapya ya Tumbelo wilayani Kondoa leo. wengine ni wachimbaji wadogo wa madini. (picha: Nyakasagani)


Dhahabu imegunduliwa katika kijiji cha  Tumbelo nje kidogo ya mji wa Kondoa, mkoani Dodoma, ambako mgodi huo umeanza kutoa madini kwa wingi na kuwafanya wachimbaji wadogo wadogo kutoka mikoa ya Tanzania kupiga kambi katika eneo hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tumbelo Gold Mine, Bw. Moshi Changai amesema mgodi huo umegunduliwa mwezi uliopita, baada ya mchimbaji mdogo wa kijiji cha Tumbelo, Bw. Hamisi Gori kugundua dhahabu hiyo.

Amesema taarifa ya kuvumbuliwa dhahabu hiyo iliwafikia wachimbaji kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania na nje ya nchi ambako wanaendelea kufurika kuchimba dhahabu hiyo.

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dodoma, Bi. Moza Said akizungumza na wachimbaji dhahabu hao aliwataka watume nafasi hiyo kujipatia ajira na mapato ya madini hayo yaboreshea maisha yao na familia zao kuondokana na umasikini. Alisema mgodi wa Tumbelo utawafanya wanananchi wa vijiji vya jirani vya Changaa, Mnenia na Bolisa, kupata ajira ya kuchimba, kupika chakula na kusafirisha abiria kwa bodaboda.

Mvumbuzi wa mgodi huo Bw. Gori amebainisha kuwa ilikuwa bahati kubwa kwake baada ya kuchimba mwamba na kusaga ambako alipata gramu 47 za dhahabu yenye thamani ya Shilingi milioni 2/- hivyo ilimlazimu kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji cha Tumbelo kuhusu ugunduzi huo, “Nimefarijika kugundua dhahabu ambayo inawasaidia Watanzaia wenzangu, naendelea kuchimba nategemea kupata dhahabu nyingi kwa sababu wachimbaji wameanza kupata dhahabu kwa wingi” alisema Bw. Gori.

Mwenyekiti wa kijiji cha Tumbelo Bw. Omari Ngarima alisema, toka mgodi huo uvumbuliwe mwezi mmoja uliopita, wachimbaji kutoka sehemu mbalimbali wamefika kuchimba madini hayo na kuiomba Serikali iwakingie kifua kwa wachimbaji wakubwa wasiwanyan’ganye mgodi kwa kisingizio cha uwekezaji.

Mnunuzi wa dhahabu hiyo, Bw. Japhet Jeremiah alisema dhahabu inayopatikana katika mgodi wa Tumbelo ni nyingi ambayo itawaletea utajiri wakazi wa wilaya ya Kondoa.
                                                   Habari na wavuti
 MTANZANIA WA KWANZA KUPANDA MLIMA EVAREST WILFRED MOSHI AWASILI NCHINI LEO.

Mtanzania wa kwanza kupanda mlima Evarest,Wilfred Moshi alipowasili nchini leo kwenye uwanja wa Kimataifa wa KIA kutoka Nchini Nepal baada ya kupanda mlima evarest ambao ni mlime mrefu kuliko yote
Mtanzania wa kwanza kupanda mlima Evarest,Wilfred Moshi(aliyevaa miwani)akiwa na watu mbalimbali akiwemo mke wake(wa tatu kulia)Agness Wilfred na watoto wake Martini na Martina Wilfred akipokelewa kwa shangwe baada ya kutoka Nchini Nepal kupanda Mlima Evarist kwa muda wa miezi ambapo alipeperusha vyema bendera ya Tanzania
Watu wake wa karibu kabisa nao walijawa na furaha ya ajabu na kujimuika pamoja wakiwa na zawadi mbalimbali kama anavyoonekana Getruda akiwa na Rodrick Mmary wakiwa na champain kwa ajili yakumzawaida Willfred
Waandishi wa habar kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kazini.

Hafla ya kumpongeza Wilfred Moshi.
Mmiliki wa mtandao huu(mwenye begi)Rodrick Mushi akimpongeza Willfred Moshi baada ya kuwasili uwanja wa KIA kutokea Nepal baada ya kufanikiwa kufika kileleni na kuwa mtanzania wa kwanza kabisa kupanda mlima evarest.
Mtanzania wa kwanza kupanda mlima Evarest,Wilfred Moshi alipowasili nchini leo kwenye uwanja wa Kimataifa wa KIA kutoka Nchini Nepal baada ya kupanda mlima evarest ambao ni mlime mrefu kuliko yote akikumbatiana na familia yake mke wake Agness Willfred na watoto wake.
Waandishi wa habari wakizungumza na mama mzazi wa Wilfred Moshi Bi Martina kuweza kuoata mawili matatu kutoka kwake.

Tuesday, May 29, 2012

KITUO CHA MSAADA WA SHERIA KUIVAA TAASISI YA RAIA WA INDIA KWA KUKIUKA HAKI ZA BINADAMU

Mwanaharakati kutoka kituo cha msaada wa sheria wanawake na watoto mkoani Iringa Bw Jackson Gaso ambaye amejitolea kupambana na raia wa India anayemiliki taasisi ya mikopo ya Brac kwa kunyanyasa wanawake Iringa
Mwanamke mjane Edina Panzi (47) siku aliyofungiwa ndani ya m,ahabusu za Brac
Hapa akichuma mbonga katika bustani yake kwa ajili ya kuuza ili aweze kulipa deni analodaiwa Brac
Sakata la mwanamke mjane Edina Panzi(47) kufungiwa katika moja kati ya ofisi za taasisi ya mikopo ya Brac tawi la Iringa taasisi inayomilikiwa na Raia wa India kwa madai ya kushindwa kulipa deni lake kiasi cha shilingi 5800 limechukua sura tofauti baada ya mwanaharakati wa kituo cha msaada wa kisheria wanawake na watoto Bw Jackson Gaso kujitosa kuifikisha taasisi hiyo mbele ya vyombo vya sheria.

Gaso amejitokeza kumsaidia mwanamke huyo kama njia ya kupinga vitendo vya unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyofanywa na taasisi hiyo ya Brac ambayo ipo chini ya raia wa India.

Hivyo amesema kuwa kituo chake kinajipanga kumfikisha mahakamani mkurugenzi wa taasisi hiyo kwa ukiukaji wa haki za binadamu kama njia ya kusaidia jamii inayonyanyaswa na taasisi hiyo.
                               Habari na Francis Godwin Iringa.

MTANZANIA WA KWANZA KUPANDA MLIMA EVAREST WILFRED MOSHI KUINGIA NCHINI LEO MAY 30.


Mtanzania wa kwanza kupanda mlima evarest ambao ni mlima mrefu kuliko yote duniani Wilfred Moshi leo anatarajiwa kuingia Nchini baada ya Kutokea Nepal ulipo mlima huo.

Akizungumza na mtandao wa www.tanzania-leo.blogsport.com mmoja wa ndugu wa karibu alisema kuwa anatarajiwa kuingia nchini majira ya saa 12:00 mchana leo.

Hata hivyo haijajulikana kama atakuwepo kiongozi yeyote wa Serikali katika kumpokea Wilfred ambaye ameitangaza vema nchini yetu duniani,ila mtandao huu ulitanabaishiwa kuwa watakuwepo familia ya Wilfred,Ndugu jamaa na marafiki.

Kwa habari zaidi endelea kufuatilia hapa www.tanzania-leo.blogsport.com

       BENKI YA RASILIMALI (TIB) YAWA MWENYEJI WA WATAALAMU WA AADFI

WAZIRI wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi za Mabenki ya Maendeleo ya Afrika (AADFI), Peter Noni kabla ya kufungua rasmi mkutano wa 38 wa mwaka wa Taasisi hiyo  jana mjini Arusha.Kulia ni Mwenyekiti wa heshima wa AADFI (Honorary Chairman) Geoffrey.





WAZIRI wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akifungua mkutano wa 38 wa mwaka wa Taasisi za Benki za Maendeleo ya Afrika (AADFI) kwenye hoteli ya Arusha palace jijini Arusha. Jopo la wataalamu kutoka Taasisi hizo wamekutana kujadili ni kwa jinsi gani wanaweza kusaidia maendeleo katika nchi za Afrika. Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) ilikuwa mwenyeji wa mkutano huo.Habari na
Grace Macha.
 
 

      MONDULI WATAKA KATIBA MPYA

MWENYEKITI WA UVCCM, MONDULI, JUILUS KALANGA WANANCHI wa Monduli wametakiwa kujitokeza kwenye mikutano ya kukusanya maoni ya katiba mpya ili waweze kutoa mapendekezo yatakayowawezesha kunufaika na rasilimali zao ikiwemo misitu na mapori yanayotumika kwa utalii wa kuwinda.
Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilayani humo, Julius Kalanga wakati alipokuwa akiwaeleza waandishi wa habari maazimio ya kikao cha kamati ya utekelezaji kilichokaa mwishoni mwa wiki .
 Alisema kuwa wilaya hiyo ina misitu na vitalu vya uwindaji wa kitalii lakini wananchi wake hawanufaiki navyo kwani malipo yote hufanyikia wizarani jambo alilosema kuwa si sahihi kwani wananchi wanaoishi kuzunguka maeneo hayo ambao huwa walinzi na hupata athari mbalimbali ikiwemo wanyama kuvamia mashamba na makazi yao hivyo wanapaswa kupata sehemu ya mapato. 
Kalanga ambaye pia ni diwani wa Nyampulukano alisema kuwa tatizo hilo linaweza kutatuliwa kwa wananchi kujitokeza kwenye mikutano ya kukusanya maoni ya katiba mpya ambapo alishauri angalau asilimia 25 mpaka 30 ya mapato ya uwindaji wa kitalii na uvunaji wa miti kwa ajili ya mbao yakarudishwa kwa jamii zinazoishi kwenye maeneo kuzunguka vitalu vya uwindaji na mazao ya misitu. 
 Aidha Mwenyekiti huyo wa UVCCM alisema kuwa wanamshukuru mbunge wao, Edward lowassa kwa kuamua kuweka wazi msimamo wake wa kutokihama chama hicho tawala kwani kabla ya hapo kulitokea sintofahamu kubwa miongoni mwa wanaCCM ambao wengine walitaka kukihama chama hicho wawahi kule ambapo waliambiwa mbunge wao atahamia.
 Pia walimpongeza Lowassa kwa kufanikiwa kutatua kero za ardhi kati ya wawekezaji na wananchi wa maeneo ya Mto wa Mbu na Meserani kwa kile alichoeleza kuwa endapo asingefanya haraka kutafutia ufumbuzi ingesababisha wananchi wengi kukikimbia chama hicho tawala. 
 “Kama wananchi wakiona hawawezi kupata haki ndani ya chama chao (CCM) watatafuta mahali pengine kwa kuipata nje ya chama chao hivyo tunamshukuru Lowassa kwa kuamua kuishughulikia migogoro hiyo ya ardhi na ufumbuzi alioupatia jambo lililosababisha wananchi kutulia” alisema kalanga.
KATIBU WA UVCCM MONDULI, EZEKIEL MOLLEL. 
 Kwa upande wake katibu wa UVCCM wilayani humo, Ezekiel Mollel alisema kuwa uchaguzi ndani ya chama hicho umeshindwa kukamilika kwenye baadhi ya maeneo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ile ya baadhi ya watendaji wa chama kutotoa fomu za kugombea huku kwenye maeneno mengine akijitokeza mgombea mmoja.
 Alisema kuwa hali hiyo imepelekea mashina 497 kati ya 2,106 wilayani humo kutofanya uchaguzi na matawi nane kati ya 72 kushindwa kufanya uchaguzi huo ambapo kwa sasa mchakato wa uchaguzi ngazi ya kata unaendelea kwa wanaCCM kuendea kuchukua fomu.
Habari na Grace Macha.
       
CUF YAWATAKA WAFUASI WAKE NA WANANCHI ZANZIBAR KUWA WATULIVU, WAVUMILIVU NA KUTOA MAWAZO YAO BILA JAZBA

Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na katibu Mkuu wa chama cha CUF Maalim Seif Sharif Hamad.
 
Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Chama cha Wananchi(CUF) kimewataka wananchi kutulia na Serikali kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha vurugu zilizotokea mwishoni mwa wiki Mjini Zanzibar.
Taraifa ya Chama hicho kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma,Salim Bimani ilisema “Chama cha CUF kinatoa wito kwa wananchi wote kuwa watulivu, wavumilivu na kuitumia fursa ya kutoa mawazo yao bila jazba na kutowanyima wengine nafasi ya kuwasilisha mawazo yao”
Taarifa hiyo ilisema kwamba vitendo vya watu wachache kuchoma makanisa moto na kuharibu mali za watu ni vya uvunjifu wa sheria na kinyume na utamaduni wa Kizanzibari.
“Uchunguzi wa kina ufanyike na waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria bila uonevu wala upendeleo” Alisema Bimani katika taarifa yake hiyo ambayo pia alisema kwamba ni lazima kwa wakati huu na kwa haraka iwezekanavyo, Serikali izungumze na Mashekhe bila ya kuona muhali na kwa uwazi kabisa ili kutafuta suluhu ya kudumu kwa faida ya nchi.
Chama hicho kimesema kwamba pamoja na sababu au visingizio mbalimbali vilivyotajwa kuwa chanzo cha hali hiyo, zikiwemo za hamasa za wananchi, chuki binafsi, ukosefu wa hekima,matumizi ya nguvu za dola na hata uchochezi wa makusudi wa wale wanaoonekana kutokupendelea maridhiano ya kisiasa Zanzibar.
“Chama cha Wananchi,CUF, kama sehemu muhimu ya Umma wa Watanzania,hakiwezi kukaa kimya kutokana na mwelekeo mzima wa hali tete ya amani katika nchi, ingawa ni dhahiri wapo baadhi ya watu wasioitakia mema Zanzibar wakibainika kufurahia mazingira hayo,kwa maslahi binafsi na pia kutoa kauli za kutatanisha za kisiasa” Alisema Bimani katika taarifa yake.
 

TANZANIA YAUNGANA NA NCHI NYINGINEZO DUNIANI KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA WALINDA AMANI WA UMOJA WA MATAIFA

 
 
Mgeni rasmi Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim na Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi. Hopolang Phororo na UwaGeneral Officer Commanding (GOC) Meja Jenerali Hassan Vuai Chema akitoa heshima zake.  wakishiriki kuimba wimbo wa taifa katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya walinda amani  Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa kila Mwaka tarehe 29 Mei. Picha zote na MO BLOG
Mgeni rasmi Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim  akiweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu ya mashujaa.
Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi. Hopolang Phororo akiweka Shada la Maua kama ishara ya kuwakumbuka walinda Amani wa Afrika.
 
MKUTANO WA KITENGO CHA URITHI WA BAHARINI ZANZIBAR
Mkuu wa Makumbusho ya Mnazi mmoja Zanzibar Ameir Ibarahim Mshenga akionesha picha ya Watafiti wa mambo ya bahari waliyofanya Zanzibar katika kikao cha k kujadili suala la uharibifu wa mambo ya bahari kilichofanyika leo ukumbi wa Makumbusho ya Kasri uliopo Forodhani
 (Picha na Iddy Haji-Maelezo Zanzíbar)
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar  
Kamishna wa Utamaduni na Michezo Zanzibar Hamadi Bakari Mshindo amesema ipo haja ya Kitengo cha Urithi wa Baharini kuwa makini na jasiri katika kusimamia vyema urithi wa Zanzibar kwani kitengo hicho kinaweza kuwa sehemu muhimu ya kuvutia watalii ambao wanaweza kuzuru maeneo ya urithi huo.
Amesema maeneo ya Urithi wa Bahari ni sehemu muhimu kwani Wageni kutoka nchi mbalimbali wamekuwa wakiyatembelea ili kujua historia ya maeneo hayo jambo ambalo linaweza kuwa kichochoe kikubwa cha kuongeza wageni ambao huja kuitembelea Zanzibar kila msimu.
Kamishna Mshindo ameyasema hayo katika kikao cha kujadili suala la uharibifu wa mambo ya bahari kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Makumbusho ya Kasri uliopo Forodhani mjini Zanzíbar.
Amesema lengo la kikao hicho ni kujadili njia nzuri za kuhifadhi urithi wa baharini ambao kama utawekewa mikakati mizuri unaweza kuisaidia Zanzíbar kupiga hatua kwani ni eneo muhimu la kuvutia watalii.
Kamishana amesema kutokana na umuhimu wake kuna haja pia ya wadau walioshiriki katika kikao hicho kuwa na mkakati wa pamoja wa kuhakikisha mazingira ya urithi huo yanahifadhiwa kwa ajili ya maslahi ya taifa.
Amefahamisha kuwa Urithi huo ni pamoja na Meli ambazo zilizama katika bahari, mapango na vitu ambavyo vimekuwa vikitupwa katika bahari mambo ambayo yanageuka kuwa urithi ambapo watu kutoka maeneo mbalimbali huwa na hamu ya kujua historia ya vitu hivyo.
Aidha urithi huo huchangia kuongezeka kwa mazalio ya viumbe hai wa bahari ambao hugeuza maeneo hayo kuwa nyumba zao za kujihifadhia na hivyo kusababisha ongezeko la samaki.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Kale Dkt.Amina Ameir amesema kuna haja ya jamii kuelimishwa juu ya umuhimu huo sambamba na kuacha tabia ya kuchukua mabaki ya urithi huo kwa lengo la kwenda kuuza mabaki hayo kwa watu wasio husika.
Amesema kuna Wazamiaji ambao hutumiwa na watu kwa lengo la kuzamua mabaki ya Meli na Mamboti ambayo yalizama na kwenda kuyafanya bishara ya chuma chakavu jambo ambalo ni kinyume na taratibu za kisheria.
Ameongeza kuwa Idara yake itachukua mkakati wa makusudi kwa kushirikiana na wadau husika kuwafahamisha wananchi kuwa Mabaki ya meli zilizozama ni urithi wa Nchi na hivyo wananchi hawana haki ya kuchukua mabaki hayo bila kupata idhini ya Kitengo cha Urithi wa Mambo ya Bahari.
Akitoa historia yake Mkuu wa kitengo hicho Fakih Othman amesema kitengo hicho kilianzishwa mwaka 2011 kikiwa na malengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya tafiti juu ya urithi wa baharini katika maeneo yote ya Visiwa vya Unguja na Pemba.
Malengo mengine ni pamoja na kushirikiana na taasisi mbalimbali za nje na ndani ya nchi zinazojishughulisha na uhifadhi na utunzaji wa urithi wa Baharini.
Fakih ametaja changamoto zinazokikabili kitengo cha Urithi wa Mambo ya Baharini kuwa ni pamoja na uhaba wa vifaa vya kufanyia kazi, ukosefu wa mafunzo pamoja na kutokuwepo kwa fungu maalum kwa ajili ya kuendeleza kitengo hicho.

    ZIARA YA WAZIRI WA NCHI AFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS      WA ZANZIBAR KATIKA KANISA LILILOCHOMWA MOTO

-Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akimuonesha Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohd Aboud maeneo yalioathirika zaidi baada ya Kanisa hilo kuchomwa moto katika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.
PICHA NA YUSSUF SIMAI MAELEZO ZANZIBAR.
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud akielezea jambo kwa Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga wakwanza kulia kuhusiana na kuchomwa moto kwa Kanisa hilo liliopo Kariakoo Mjini Zanzibar katikati ni  Mkuu wa Jeshi la Polisi I,G,P Saidi Mwemwa.
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akielezea  kwa Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud na Viongozi wengine mbalimbali kile kilichotokea baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akibubujikwa na Machozi kwa kuguswa na hotuba iliokuwa ikitolewa na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tukio hilo.
-Mkuu wa Dini ya Kiislam Afisi ya Mufti wa Zanzibar Thabit Noman Jongo akitoa hotuba ya Dini inavyoeleza kuhusiana na kudumisha Amani na Usalama katika nchi na kuondosha mifarakano na chuki na kuharibu mali.Katika kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar ambalo limechomwa moto.
Mku wa Jeshi la Polisi I,G,P Saidi Mwema akitoa hotuba kwa Maaskofu na baadhi ya waumini wa Kikristo katika kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar lililochomwa moto,ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.kuliani kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Abdalla Mwinyi na kushoto yake ni Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Abdalla Mwinyi Khamis akitoa hotuba na kuonyesha Umoja na Mshikamano uliokuwepo kati ya Waislam na Wakristo kwa Picha ambayo imebuniwa na Mchoraji wa kingereza na kuwataka kuendelea na mshikamano wao ili kuzidi kuleta amani nchini.
habari na fullshangwe

MADIWANI MOSHI VIJIJINI WAMTUHUMU MBUNGE WA MOSHI VIJIJINI CYRIL CHAMI.

Mbunge wa Moshi Vijijini Cyril Chami(katikati)akifuatilia hoja kwenye baraza la madiwani.

Diwani akitoa hoja kwenye kiako hicho cha baraza kilichofanyika leo.  


BARAZA la madiwai wa halmashauri ya wilaya ya Moshi, mkoani
Kilimanjaro, limeelezwa kuwa wabunge wanaopaswa kuhudhuria kwenye
vikao vya baraza hilo, wanaongoza kwa utoro hivyo kutokuwa na
uwakilishi wa kutosha katika vikao hivyo.

Hoja hiyo ilitolewa jana na diwani wa kata ya Arusha-chini (TPC),

Rojas Mmari, alipokuwa akitoa hoja za maswali 10, aliyowasilisha
kwenye kikao cha baraza la madiwani kilikutana jana katika ukumbi wa
halmashauri hiyo wilayani hapa.

Wabunge waliotajwa ni pamoja na Dk. Cyrill Chami wa Moshi vijijini,

Dk. Augustine Mrema wa Vunjo na mbunge wa viti maalum mkoani
Kilimanjaro Betty Machangu, ambao kwa mujibu wa diwani huyo wamepata
kuhudhuria vikao vichache katika kipindi cha miaka miwili tangu
uchaguzi wa mwaka 2010.

Akizungumzia hilo diwani Mmari alisema ni vyema baraza lijulishwe

sababu za wabunge hao kushindwa kuhudhuria kwenye vikao vya baraza
hilo kuliko hali ilivyo, na kusema kuwa jambo hilo ni moja ya
ukiukwaji wa taratibu na kanuni za baraza zinazozungumzia mahudhurio
ya wajumbe wake kwenye vikao hivyo.

Mbali na hilo Mmari alirusha tuhuma kwa mbunge wa jimbo la Moshi

vijijini Dk. Chami, ya kwamba amekuwa aitumia magari ya halmashauri
kwa ajili ya ziara ya kutembelea wapigakura wake kwenye jimbo,
akitolea mfano wa ziara yake ya mwisho ambapo alitumia gari la
mkurugenzi wa halmashauri hiyo.

Hoja hiyo ilipingwa vikali na Dk. Chami, ambaye alitaka baraza hilo

kuunda tume ya kuchunguza tuhuma zilizotolewa na diwani huyo dhidi
yake ili kuweka wazi kile kinacholalamikiwa dhidi yake.

“Mh. Mwenyekiti naomba tume iundwe ili ukweli ubainike maana hakuna

siku hata moja niliyotumia gari la halmashauri kwa ajili ya ziara
zangu kwenye kata, lakini mtoa hoja atueleze ni hatua gani zichukuliwe
pale diwani anaposema uongo mbele ya baraza hili”, alisema Dk. Chami.

“Mwenyekiti naomba kukanusha sijawahi kutumia gari la halmashauri

kutembelea kwenye kata zangu”, alisema Dk. Chami, ambaye alifanya
ziara ya mwisho jimboni humo mwezi mmoja kabla ya kuvuliwa madaraka ya
uwaziri katika mabadiliko yaliyofanywa hivi karibuni na rais Kikwete
kwa kuzingatia ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za
serikali iliyobaini dosari mbali mbali katika shirika la viwango
nchini (TBS), lililoko chini ya wizara hiyo.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Moshi Moris Makoi, wakati

akihitimisha hoja hiyo, alisema kuwa ni kweli kuwa gari la mkurugenzi
wa halmashauri hiyo, lilitumika kwenye ziara ya mwisho ya mbunge huyo,
lakini liliwabeba baadhi ya watumishi wa halmashauri na sio mbunge
kama ilivyodaiwa na diwani huyo.

Hata hivyo alisema hoja hiyo haipaswi kuendelezwa kwenye kikao hicho

kwa tahadhari ya kuibua mvutano na malumbano yanayoweza kukwamisha
mijadala mingine kulingana na ratiba ya kikao hicho.

Katika hatua nyingine kikao hicho cha madiwani kilielezwa kuwa ofisi

ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo na eneo la mapumziko na
vikao vya madiwani haijakamilika kutokana na chumba kilichotengwa
kuendelea kutumika kuhifadhi masanduku ya kupigia kura.

Hoja hiyo ni sehemu ya zile zilizotolewa na diwani Mmari, ambaye

alisema mpaka sasa madiwani wameonekana wakishinda kwenye korido za
jengo la halmashauri hiyo bila kuwa na eneo maalum la kuendesha
shughuli zao, ikiwemo mipango mbali mbali inayopaswa kusimamiwa na
madiwani hao.

Katika hoja yake hiyo Mmari alipendekeza ofisi hiyo ya mwenyekiti

kukarabatiwa na kuwa na vitendeakazi vya kisasa kwa kutambua uzito wa
kiongozi huyo kwenye halmashauri hiyo.

      Uzinduzi rasmi wa tawi la Chadema Washington Dc wafanyika

 

Uongozi wa juu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  katika uzinduzi rasmi watawi la Chadema Washington Dc  kwenye meza ya juu wa kwanza kushoto Libe Mwangombe, akifatiwa na Mhe. Peter Msigwa,  Mwenyekiti wa tawi Mhe. Kalley Pandukizi,  Mhe. Zitto Kabwe, na Mhe. Nassari Joshua, Dogo Janja, mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Mirage Hall uliopo University Of Bld, Hysattsville, Maryland Nchini Marekani.f
Mhe. Zitto Kabwe akitoa hutba kuelezea mpango mzima wa mambo yanavyoendelea nchini Tanzania
Wantazania waishio DMV Nchini Marekani wakiwa katika uzinduzi wa tawi la chadema Washington  Dc
Wantazania waishio DMV Nchini Marekani wakiwa katika uzinduzi wa tawi la chadema Washington  Dc
                                                             Habari na Fullshangwe.

WATU 30 WAPANDISHWA KIZIMBANI ZANZIBAR KWA KUDAIWA KUHUSIKA NA VURUGU NA KUHARIBU MALI


Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Watu 30 wakiwemo wanaosadikiwa kuwa  wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam  wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe  wakikabiliwa na makosa mbalimbali ikiwemo kuwashambulia Polisi,kuchoma moto matairi ya Magali barabarani na ukorofi.
Mbali na tuhuma hizo,pia wameshtakiwa kwa kufanya maandamano yasiyokuwa na kibali kinyume na sheria  pamoja na  uzembe na ukorofi wa kuwashambuliya polisi kwa mawe.
Watuhumiwa hao walifikishwa katika mahakama nne tofauti, ikiwemo mahakama ya hakimu Mohammed Ali Mohammed walikofikishwa watuhumiwa wawili, wanne kwa hakimu Janet Nora Sekihola, 11 kwa hakimu Omar Mcha Hamza na 11 waliobakia, wamepandishwa mbele ya hakimu Valentine Andrew Katema.
Kwa nyakati tofauti watuhumiwa hao walishitakiwa kwa makosa ya kufanya mikusanyiko isivyo halali, uzembe na ukorofi pamoja kufanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani.
Watuhumiwa hao ni Mbarouk Said Khalfani (45), na Mussa Juma Issa (57) wanaodaiwa kuwa ni viongozi wa Jumuiya hiyo, ambapo walifikishwa mbele ya hakimu Mohammed Ali Mohammed, na kusomewa shitaka la kufanya mkusanyiko isivyo halali kinyume na kifungu cha 55 (1) (2) (3) na kifungu cha 56 cha sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.
Wengine ni Mbwana Hamadi Juma (50), Massoud Hamadi Mohammed (17), Mohammed Juma Salum (35), Abdulrahman Simai Khatib (19), Hashim Juma Issa (54) Matar Fadhil Issa (54).
MENEJA WA SHIRIKA LA BIMA TAWI LA MOSHI MKOANI KILIMANJARO AWATAKA WATUMISHI WA SERIKALI,WAFANYABIASHARA NA WATU BINAFSI KUJIUNGA NA BIMA HIYO.
Meneja wa shirika la bima ya taifa tawi la Moshi Mkoani Kilimanjaro John Mdenye akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake.

Waandishi wa habari(kushoto)venance Maleli wa radio moshi Fm na Gift Mongi wakimsikiliza Meneja wa Shirika la Bima ya Taifa(hayuko pichani) .

 Meneja wa shirika la bima ya taifa tawi la Moshi Mkoani Kilimanjaro John Mdenye akifafanua jambo.

Meneja wa shirika la bima ya taifa tawi la Moshi Mkoani Kilimanjaro John Mdenye amewataka watumishi wa Serikali,wafanyabishara na wadau wengine kujiunga na bima hiyo huku akisema kuwa shirika hilo kwa sasa linafanya vizuri baada ya kulipa ,madai yote ya wanachama waliokuwa wanadai kutoka Wilaya sita za Mkoa wa Kilimanjaro.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mdeye alisema kuwa malalamiko yaliyokuwepo kwa shirika hilo yalikwishafanyiwa kazi kwa fedha za wadai  kuwa tayari lakini wakati shirika hilo zilipotembea maeneo mbalimbali hawakuweza kuonana nao lakini wadai wote wa tangu mwaka 2009 wamekwishalipwa.

Alisema kuwa kama wapo ambao wanalalamika kuwa hawajalipwa fedha zao zipo tayari na kinachotakiwa ni kufika kwenye shirika hilo la bila.

Hata hivyo aliwataka Walimu wanaopenda mkopo kwenye taasisi za fedha za kijamii kujiunga na bima hiyo kutokana na utofauti mkubwa uliopo baina  taasisi hizo za kifedha za kijamii shirika hilo la bima ya taifa.

Alisema mwenendo wa shirika hilo kwa sasa ni mzuri tofauti na miaka 1996 ambapo alieleza changamoto zilizokuwepo kwa kipindi hicho kuwa ni pamoja na soko huru (liberalization) na kuchangia kuwepo kwa ushidnani mkubwa kwa taasisi binafsi zilizojihusisha na na utoaji huduma wa bila.

“Hali ya shirika la Bima ni nzuri kwasasa na  tangu mwaka 2009 shuka chini hakuna madai yoyote na kama yapo basi ni wale waliohama maeneo au kushindwa kufika kuchukua madai yao ambapo Meneja huyo aliwataka kufika kwenye shirika hilo ili kuchukua madai yao”Alisema  Mdenye.

Alibainisha kuwa  zaidi ya shilingi billion 935 zimeweza kulipa madai yaliyokuwepo kwa wadai na kubainisha kuwa miaka ya 2009 kurudi nyuma madai hayo  yalichangiwa na shirika kukabiliwa na changamoto ya kuwepo kwa maradhi mengi ikiwemo UKIMWI ambayo yalichangia kuwepo kwa vifo vingi.

Kwa upande wa mawakala wanaojishughulisha na masuala ya bima ambao wamekuwa wakisababisha usumbufu mkubwa kwa wateja alisema mawakala hao wanawajibu wa kuwaelimisha wateja umuhimu wa kujiunga pamoja na huduma mbalimbali za bima,lakini kama watakuwa wanafanya kinyume wakibainika watachukua hatua za kisheria.