AFISA ELIMU WA MKOA WA MBEYA JU
WALIMU wapatao 19 mkoani Mbeya wamegundulika
kuwa waligushi vyeti vya shule kabla ya kuajiliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya ufundi nchini.
Uchunguzi uliofanywa kwa ushirikiano
mkubwa na baadhi ya watumishi wa idara ya elimu katika ngazi mbalimbali
umebaini kuwepo kwa udanganyifu wa vyeti kwa baadhi ya walimu huku baadhi
wakiwa wamenunua vyeti hivyo wengine kuopewa na ndugu zao ambao tayari nao
wameajiriwa na Serikali.
Baadhi ya majina ya walimu
waliogushi vyeti vya masomo yao ni pamoja na Mwalimu Omary Shaban Isingo kutoka
wilaya ya Chunya, Vumilia Petro Pangani Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Lucy M.
Amulike kutoka Ileje, Atuganile Mateo Mwakibete Jiji la Mbeya, Seif M.
Rwambo kutoka Kyela na Elizabeth Isaya kutoka wilaya ya Mbozizote za mkoani
hapa.
Wengine ni Mwalimu Frida M. Edward
ambaye vyeti vyake vimerekebishwa majina kutoka wilaya ya Mbarali, Jenifer
Semeni Kahangwa kutoka Mbeya Vijijini ambaye hana taarifa za Wizara, Ezekiel
Longnus Mchembe kutoka Mbozi, Nsoma John Guyashi kutoka Mbeya Vijijini na
Zawadi Andason Ndelwa kutoka wilaya ya Mbozi.
Walimu wengine waliothibitishwa na
Ofisi ya Rais, tume ya utumishi wa umma idara ya utumushi wa walimu ni Betty
Osmund Mchombe kutoka Mbozi, Janeth Attilio Mvanda kutoka Mbozi, Amos Stephen
Mwasabila kutoka Mbozi, Ritha B. Ndaka kutoka Mbozi, Chrispin S. Vungwa kutoka
Mbozi, Fatuma S. Mgude kutoka Rungwe, Faida J. Mwampir kutoka Mbozi na Faida A.
Mwampira kutoka wilaya ya Mbozi.
Orodha ya Majina hayo pia
imepelekewa tume ya ya Utumishi wa umma idara ya utumishi wa walimu mkoani hapa
chini ya G.K Mbilinyi.
Licha ya walimu hao majina yao
kupelekwa kwa viongozi wanaohusika mwaka mmoja uliopita, hakuna hatua zozote za
kisheria na kinidhamu zilizochukuliwa dhidi yao.
Hata hivyo imeelezwa kuwa pamoja na
orodha hiyo pia kuna baadhi ya walimu ambao baadhi ni watoto wa vigogo wa
viongoai waliokuwa idara ya elimu ambao nao wanasadikiwa kugushi lakini wao
wamekuwa hawaguswi na tuhuma hizo.
Pamoja na madhara hayo kuukabili
mkoa wa Mbeya kwa upande wa walimu, madhara mengine ni pamoja na Utoro kazini
kwa walimu na walimu wa kiume kufanya mapenzi na wanafunzi wa kike.
Sanjari na changamoto hiyo,
changamoto nyingine inayoikabili idara ya elimu mkoani Mbeya ni baadhi ya
waratibu elimu Kata ambao bado hawajawafikia kikamilifu walimu na muda mrefu wanautumia
ofisini kana kwamba wapo likizo.\
Hapari na Gordon Kalulumba Mbeya.
|
No comments:
Post a Comment