WAGOMBANIA MAITI |
PICHA YA MAZISHI(CYO HALISIA)
Mtafaruku mkubwa umeibuka wa kugombania maiti, kati ya ndugu wa marehemu na aliyekuwa mume wake, huku dada wa marehemu akidai kadi za benk na mwajiri akihitaji vyombo vya ndani kwa madai kuwa fedha zilizonunulia alimkopesha kazini Marehemu aliyetambulika kwa jina la Rahima Hamard mwenye umri wa miaka 24, alifariki March 4 katika hosptali ya rufaa ya KCMC baada ya kujifungua mtoto ambaye alikuwa hajatimiza siku “njiti”, katika hosptali ya rufaa ya KCMC iliyopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. Akizungumza na blog hii mume wa marehemu Matheo Juma alilieleza kuwa yeye na mkewe ambaye kwasasa ni marehemu waliishi nae kwa kipindi cha mika sita, lakini chakusikitisha ni kwamba upande wa familia ya marehumu wamekana kutomtambua. Alisema kuwa awali ndugu wa mkewe walikuwa wakifika nyumbani kwake na kupata malazi, lakini baada ya kutokea kifo hicho wamemkana kutomtambua na kudai kuwa marehemu hakuwa na mume hivyo mazishi hayawezi kufanyika sehemu nyingine tofauti na alipozaliwa kijijini kwao Rombo. Juma alisema kuwa wakati akiishi awali mkewe alikuwa ni mkirito, na alibadilisha dini kwa ridhaa yake bila kushinikizwa na kuwa mwislamu, hali iliyopelekeakutambulishwa kwa wazazi wa mwanamke kueleza mikakakati ya kufunga ndoa naye. Alisemakuwa mara baada ya msiba kutokea kaka wa marehemu Doe Swai amekata kutomfahamu na kusema kuwa dada yao hakuwa na mume hukuakimtumu yeye ndiye anahusika na kifo hicho kutokana na ujauzito,hivyo mwili huo lazima uzikwe kwa kufuata misingi ya dini ya Ukristo. Juma alisema mbali na hilo, pia dada wa marehemu aliyetambulika kwa jila la Eliza na aliyekuwa mwajiri wa marehemu Stella Sembeti, wamekuwa wakidai mali zilizoachwa na marehe vikiwemo vyombo vya ndani,kadi za benk pamoja na nguo, ikiwa hadi sasa mazishi hayajafanyika. Alisema kutokana na hali hiyo pia ametishiwa maisha endapo atahudhiria mazishi na kama ataendelea kuun'gan'gania mwili wa marehemu, na kueleza hapo awali marehemu aliwahi kugombana na dada yake Eliza na kumkataza kufika nyimbani kwake na kutohudhuria mazishi yake lakini amekuwa wa kwanza kuhitaji kadi za benk. Kwa upande wao majirani wa marehemu alilieleza gazeti hili kuwa wakati mwajiri na dada wa marehemu walifika kudai mali hizo, wananchi wenye hasira kali walijikusanya kwa lengo la kuwapiga lakini fujo hizo zilitulizwa na mwenyekiti wa serikali za mitaa na kuamuru vyombo hivyo vihamihwe ili viwekwe sehemu yenye usalama kwa usimamizi wake. Akizungumza na mwandishi wa habari hii kwa njia ya simu dada wa mareheme Eliza alikiri kuwapo kwa mvutano huo, na kueleza kuwa hawezi kumtambua mwanaume aliyekuwa akiishi naye kwani hana cheti cha ndoa, na kwamila za wachaga haziruhusu azikwe nje ya familia. Eliza alisema kuwa uamuzi wa kumzika marehemu nyumbani kwa wazazi wake ni kutokana na wosia alioundika marehemu pamoja na kuwaeleza watoto wake kuwa endapo akifariki azikwe kwa baba na mama yake. Alisema kuwa mbali na hayo hawezi kumtambua kwasasabu hajawahi kutoa mahari yeyote, hivyo hana uhalali na mwili wa marehemu, huku akidai kuwa mali zote ni za marehemu kwa mume huyo hakuwa na kitu chochote tangu walipoanza kuishi. Eliza alieleza kuwa marehemua alikuwa amolewa na mwanaume mwingine tena kwa kufunga ndoa katika kanisa la katholiki mbele ya padri, hiyo anayedai kuwa alikuwa mume wake kwasasa alimn’yan’ganya mwanaume mwingine hivyo akaamishia mali zote kwake. Akizungumzia kuhusu mali anazozidai, Eliza alisema kuwa mali zote ni zadada yao marehemu, na kudai kuwa kadi ya benk marehemu aliisafirisha mbali kusikojulikana, ambapo wakati mazungumzo yakiendelea Eliza alinyan’ganywa simu na mtu aliyebainika kuwa wa kiume na kusema hapa tupo kwenye msiba, na kukata simu na kuizima. alilifanikiwa kumpata aliyekuwa mwajiri wa marehemua Stella Sembeti na kukiri kuwa marehemu alikuwa mfanyakazi wake katika hoteli ya Kiusa Pabu kama meneja wa hoteli hiyo iliypo mjini moshi |
Sunday, March 18, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment