Saturday, April 14, 2012

Picha ya Wikiend,wadau kwa staili hii ntamshangaa sana mtu anayemtukana mama.

Mama aliyebeba watoto wawili kama inavyoonekana kwenye picha ambaye jina lake halikuweza kupatikana kama alivyokutwa na kamera yetu maeneo ya Kibosho Wilaya ya Moshi Vijijini.


Chakushangaza au wanavyodai wahusika mfumo dume katika maeneo hayo bado unaendelea kupewa nafasi,ikiwemo wanawake kutokuwa na haki ya kukutana na wanawake wenzao,kuunda vikundi au kumuuliza mume wake kwa nini wamechelewa.


Hivyo wadau wanaohusika na harakati za ukombozi wa wanawake na watoto walioko pembezeni ni vema wakaweka nguvu zaidi maeneo ya vijijini tofauti na kufanya harakati hizo maeneo ya mjini na huku vijijini wahusika wakiwa wanateseka.


No comments:

Post a Comment