Monday, April 8, 2013

KIKULETWA KUFUFULIWA JE CHUO CHA ARUSHA KITAWEZA KUZALISHA UMEME KAMA ILIVYOKUWA APO AWALI??


Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama(Katikati) akipata maelezo ya Kituo cha Kuzalisha umeme cha Kikuletwa kilichopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kutoka kwa Mtaalamu wa Chuo cha Ufundi Arusha,Aliyesimama nyuma ya mkuu wa mkoa mwenye miwani ni mkuu wa chuo hicho Dk Richard Masika


Chuo cha Ufundi Arusha kimeanza mkakati wa kufufua mitambo ya kuzalishia umeme wa maji wa Kituo cha Kikuletwa iliyopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro ambapo hadi itakapokamilika itaweza kutosheleza mahitaji ya mikoa ya Kilimanjaro na Arusha na umeme mwingine kubaki.

Ufafanuzi huo umetolewa na  mkuu wa Chuo hicho Dk Richard Masika kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama aliyetembelea mitambo hiyo ambayo imekabidhiwa kwa chuo hicho na Shirika la Umeme Nchini(TANESCO)

Alisema kuwa chuo hicho ambach kitakuwa cha kwanza barani Afrika kumiliki kituo cha kufua umeme,kitatumia kituo hicho kwa malengo matatu ambayo ameyataja kuwa ni pamoja na kutumika kwa mafunzo,kutengeneza vipuri vya mitambo ya umeme pamoja na kuzalisha umeme.

Dk Masika ameeleza kuwa baada ya kukabidhiwa kituo hicho mapema wiki iliyopita na baadaye kuanza kazi za awali wamebaini kwamba kwa kufunga mitambo mipya ya kufua umeme wataweza kutoa megawati 17 ambazo zitaingizwa katika gridi ya taifa.

“Kiasi hicho kitaweza kutosheleza mahitaji ya umeme kwa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha na kiasi kingine kubaki,”

Akifafanua zaidi alisema kuwa kituo hicho ambacho kilijengwa mwaka 1930 kwa sasa kina mashine tatu ambazo zilikufa na kuacha kuzalisha umeme mwishoni mwa miaka ya Themanini zikiwa na uwezo wa kuzalisha umeme kati ya megawati moja na moja na nusu.

Dk Masika ameeleza kuwa mashine mbili kati ya hizo tatu chuo chake kina uwezo wa kuzifufua na kuanza kufua umeme utakaoingizwa katika gridi ya taifa wakati chuo chake kikiendelea na mkakati wa mpango mkubwa wa uzalishaji umeme kwa kutumia mitambo ya kisasa

Kwa upande wa mafunzo,Dk Masika ameeleza kuwa cuo hicho kimelenga kutoa idadi kubwa ya wataalamu wafanyakazi ambao wenye taalamu ya stashahada ambao kwa kawaida ndiyo wacahapa kazi ili kuzipa pengo la sasa la idadi kubwa kukimbilia katika shahada na baada ya kuhitimu kwa wasimamizi na si wachapa kazi

Alisema kuwa mitambo ya kituo hicho chenye eneo la jumla ya Ekari 400 yanategemea maji ya mito miwili ambayo Kware unaoanzia Mlima Kilimanjaro na Mto Mbuguni unaonzia mlima Meru ambapo maji hayo huduma katika kipindi kizima cha mwaka na kuongezeka wakati wa kiangazi

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kilimanajro,Gama amewataka wataalamu wa cuo hicho pamoja na mipango mizuri na kuonyesha kuwa na uwezo mkubwa wa kukiendesha lakini aliwataka kuwa na uzalendo ambao utalisaidia taifa katika kutatua tatizo la upatikanaji wa nishati ya umeme.

Alisema kuwa ni vyema sasa wakatambua kwamba taifa limewapa dhamana kubwa kwa kuwakabidhi raslimali kubwa ambayo inatakiwa kusimamiwa vyema kwa ajili ya manufaa ya watanzania na siyo ya watu binafsi.

Gama aliwataka kuhakikisha wanatunza vyanzo vya maji yanayotumika katika mitambo hiyo vya Chemka kilichopo wilayani Hai na cha Mto Mbuguni ambacho kipo wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Alisema kuwa uongozi wa serikali mkoani Kilimanjaro unakiweka kituo hicho katika miradi yake mikubwa ya kimkoa na utakuwa tayari kikusaidia chuo hicho wakati wowote kitakapohitaji msaada wa hali na mali.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga ameahidi kukipa ushirikiano chuo hicho na kukitaka kuhakikisha kinaimarisha kitengo chake cha uhusiano ili kujenga mahusiano na vijiji vinavyozunguka kituo hicho.

Alisema kuwa kutokana na mazingira yanayozunguka kituo hicho kutunzwa vizuri katika miaka yote tangu uzalishaji uliposiamama,mara nyingine wakati wa ukame mkali baadhi ya wenyeji ujaribu kuingiza mifugo kwa ajili ya kupata malisho na hivyo kusababisha vurugu.

Makunga alisema kuwa ni vyema chuo hicho kikajipanga kwa kushirikiana na uongozi wa wilaya katika kuhakikisha kinawaelimisha wananchi wanaoishi maeneo ya jirani ili watambue umuhimu wa kituo hicho na madhara ya kutaka kuingiza mifugo kwa nguvu

No comments:

Post a Comment