Tuesday, March 5, 2013

BREAKING NEEEWS"MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAHARIRI ABSALOM KIBANDA AVAMIWA NA KUJERUHIWA VIBAYA.

 

 Pichani ni Nduge Absalom Kibanda akiwa amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mkuu wa New Habari Cooperation Absalom  Kibanda amevamiwa usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Mbezi Beach na watu wanasiojulikana na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili.

Inaelezwa kuwa baada ya tukio hilo Kibanda alikimbizwa katika hospitali ya Muhimbili ambapo anaendelea kupata matibabu licha ya kupata majeraha makubwa kichwani na sehemu ya jicho.

Habari hizi ni za kushtukiza na za kusikitisha ila tuzidi kumuombea Mungu amponye ndugu yetu rafiki yetu mpambanaji Kibanda.

No comments:

Post a Comment