KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI TIGO KUTOA VIFAA VYA NISHATI YA JUA KWA AJILI YA KUCHAJIA SIMU

Balozi wa kinywaji cha Hennessy kukutana na wafanyabiashara

……………………………
Na Mwandishi wetu
Balozi wa kinywaji cha Hennessy,
Cyrile Gautier Auriol, yupo nchini kwa ajili ya shughuli mbali mbali
pamoja na kukutana na wafanyabiashara wa jiji la Dar es Salaam.
Auriol aliwasili jijini leo na
kufanya mazungumza na wenyeji wake kabla ya kuelezea nia ya safari yake
ambayo lengo kubwa ni kutanua soko la kinywaji hicho maarufu duniani kwa
Watanzania nan chi za Afrika Mashariki.
Alisema kuwa pamoja na kukutana
na wafanyabiashara, pia atakutana na watu wa sekta tofauti, miongoni
mwao ni wanamuziki na wanamitindo. Ziara ya balozi huyo itakuwa ya siku
tano.
Alifafanua kuwa ujio wake ni
mara ya pili kwa ukanda wa Afrika Mashariki na ameona kuna mafanikio
makubwa kwa wafanyabiashara na hasa katika soko la vinywaji vikali.
Alisema kuwa kinywaji cha
Hennessy kwa sasa ndicho kinatamba katika ukanda huu na hivyo kuna haja
kwa Watanzania kuanza kupartavradha kwa ajili ya kujenga mwili na afya
bora. Ikiwa na zaidi ya historia ya miaka 250, Hennessy inatajwa kuwa
kinywaji (Cognac) bora zaidi duniani.
Pia Auriol atakutana na wapenzi
wa Hennessy katika matukio mbalimbali maalumu ikiwemo chakula cha mchana
katika hoteli ya Hyatt Regency ambapo baadhi ya wanawake
watakaochaguliwa watapata fursa ya kujifunza historia ya kinywaji cha
Hennessy lakini pia kuonja aina mbalimbali za kinywaji hicho lengo
likiwa kuwafundisha wanawake namna ya kufurahia kinywaji hicho wakiwa
majumbani mwao.
Balozi Auriol pia atahudhuria
chakula cha jioni na wafanyabiashara wa hapa nchini katika mgahawa wa
Akemi uliopo katika ghorofa la Diamond Jubilee. Balozi Auriol atatoa
elimu kuhusu Hennessy ikifuatiwa na uonjaji wa kinywaji hicho pamoja na
chakula kitakachoandaliwa na mpishi mkuu wa hotel hiyo.
Ziara ya balozi Auriol inaenda
sambamba na juhudi nyingine za kutangaza kinywaji hicho hapa nchini,
mojawapo ikiwa ni kampeni ya mabango ya ‘Flaunt Your Taste’ yaliyosambaa
jiji zima pamoja na ukamilishaji wa chumba cha Hennessy kilicho katika
Club 327, ambacho balozi Auriol atakizindua.
Balozi Auriol atakuwa na kikao
maalumu pia na wapenzi wakubwa wa kinywaji hicho, na pia atawazawadia
mialiko maalumu ya kuingia kwenye klabu ya wapenzi wa kinywaji hicho ya
Afrika mashariki.
Pia atatoa mafunzo maalumu kwa
baadhi ya wahudumu kutoka katika bar kubwa za jijini. Lengo kuu la
mafunzo hayo yatakayofanyika katika hoteli ya Southern Sun na George
& Dragon ni kuwapa wahudumu ujuzi utakaowawezesha kutoa huduma bora
na ya kipekee kwa wateja wao wakati wakiburudika na kinywaji cha
Hennessy kwenye bar au hotel wanazozipendelea.
Matukio ya uchaguzi wa CCM mjini Dodoma leo



GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ SEASON 2 KEY MESSAGES – EA

Guinness® is calling upon
football fans to play for their country in the new Pan-African show, as
contestants from Kenya, Tanzania, Uganda, Cameroun and Ghana go
head-to-head
Successful teams could win up to
900,000 USD in Season 2, as contestants represent their nation to find
out who is Made of More and has the skill and knowledge to go all the
way and be crowned Pan-African champions
In the new Season even more
people can get involved in the GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ in a number
of different ways. Alongside the exciting new TV show there will be
the return of the GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ mobile phone game so
that fans can test their football trivia on their mobile phone; and live
GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ quizzes in bars
AUDITION EVENTS
Guinness® is searching for
football lovers who have what it takes to represent Tanzania on a
Pan-African stage, and show that they can achieve their potential and be
recognised as players, rather than spectators in life
Players can try out for a chance
to appear in the show at the GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ audition
events. Three events to search for the stars of Season 2 of the
GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ will be held in:
At Leaders Club, Dar es Salaam on 24th November
Teams of two football fans who
think they have the brains and the brawn to step up and represent
Tanzania in the GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ should come along and try
out for the show. One of you will need to demonstrate great skill with a
ball at your feet, and your partner should know everything there is to
know about the beautiful game. You will be put through your paces in a
series of challenges to see if you could represent your nation and be in
with a chance of winning up to 900,000 USD.
The GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™
audition events will be a fun day out for everyone, with football
activities, music and entertainment. Entry is free but will be
restricted to only those 18+.
WADAU ZANZIBAR WAOMBWA KUCHANGIA SHULE ZA KATA TEMEKE DSM

(Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar)
…………………………………………….
Na Mwanaisha Mohammed-Maelezo Zanzibar
Wadau na Makampuni mbali mbali
Zanzibar wameombwa kuichangia Taasisi ya ‘Cooperation for assisting
handicapped people’ inayojishughulisha na kusaidia watu wasiojiweza ili
Taasisi hiyo iweze kujenga Mabweni ya Shule mbili za kata Temeke Jijini
Dar es Salaam.
Ombi hilo limetolewa na
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni hiyo Mhina Michael Shengena wakati
alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya
Habari Maelezo Rahaleo Mjini Zanzibar.
Amesema wanahitaji wasaidiwe Sh
Milioni Arobaini (40,000,000) ndani na nje ya Zanzibar kwa ajili ya
ujenzi wa Mabweni ya watoto Yatima,Walemavu na Watoto wanaoishi katika
mazingira hatarishi ili waweze kupata taaluma ambayo itawasaidia katika
maisha yao.
Amezitaja Shule ambazo wana
mpango wa kujenga mabweni kwa wanafunzi hao kuwa ni Nguva na Sumangira
zilizopo katika Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
Aidha
ametaja njia ambayo Wadau mbalimbali wanaweza kuchangia msaada wao kwa
Kampuni hiyo kufanikisha ujenzi huo kuwa ni kupitia akauti namba
01J2070153800 ya CRDB Bank.
Mkurugenzi
Mhina ameongeza kuwa watakuwa na ziara ya nchi nzima ambapo wanatarajia
kukutana na Viongozi wa Serikali, Siasa, Dini na Wananchi mbali mbali
katika kuitangaza Taasisi yao ili wadau waweze kuifahamu na kuichangia.
Aidha ametoa wito wa wananchi wa Zanzibar kushiriki katika harambee ya
kuichangia Taasisi yao itakayofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani
January 30, mwaka 2013 mjini Zanzibar.
Taasisi
ya ‘Cooperation for assisting handicapped people’ yenye Makao Makuu
yake Mkoani Iringa imesajiliwa mwaka 1998 chini ya Sheria za makampuni
ya Tanzania Bara na kupewa namba za usajili 3388 ambapo shughuli yake
kuu ni kusaidia watu wasiojiweza.
habari picha na bukuku blog.
No comments:
Post a Comment