Tuesday, May 29, 2012

MENEJA WA SHIRIKA LA BIMA TAWI LA MOSHI MKOANI KILIMANJARO AWATAKA WATUMISHI WA SERIKALI,WAFANYABIASHARA NA WATU BINAFSI KUJIUNGA NA BIMA HIYO.
Meneja wa shirika la bima ya taifa tawi la Moshi Mkoani Kilimanjaro John Mdenye akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake.

Waandishi wa habari(kushoto)venance Maleli wa radio moshi Fm na Gift Mongi wakimsikiliza Meneja wa Shirika la Bima ya Taifa(hayuko pichani) .

 Meneja wa shirika la bima ya taifa tawi la Moshi Mkoani Kilimanjaro John Mdenye akifafanua jambo.

Meneja wa shirika la bima ya taifa tawi la Moshi Mkoani Kilimanjaro John Mdenye amewataka watumishi wa Serikali,wafanyabishara na wadau wengine kujiunga na bima hiyo huku akisema kuwa shirika hilo kwa sasa linafanya vizuri baada ya kulipa ,madai yote ya wanachama waliokuwa wanadai kutoka Wilaya sita za Mkoa wa Kilimanjaro.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mdeye alisema kuwa malalamiko yaliyokuwepo kwa shirika hilo yalikwishafanyiwa kazi kwa fedha za wadai  kuwa tayari lakini wakati shirika hilo zilipotembea maeneo mbalimbali hawakuweza kuonana nao lakini wadai wote wa tangu mwaka 2009 wamekwishalipwa.

Alisema kuwa kama wapo ambao wanalalamika kuwa hawajalipwa fedha zao zipo tayari na kinachotakiwa ni kufika kwenye shirika hilo la bila.

Hata hivyo aliwataka Walimu wanaopenda mkopo kwenye taasisi za fedha za kijamii kujiunga na bima hiyo kutokana na utofauti mkubwa uliopo baina  taasisi hizo za kifedha za kijamii shirika hilo la bima ya taifa.

Alisema mwenendo wa shirika hilo kwa sasa ni mzuri tofauti na miaka 1996 ambapo alieleza changamoto zilizokuwepo kwa kipindi hicho kuwa ni pamoja na soko huru (liberalization) na kuchangia kuwepo kwa ushidnani mkubwa kwa taasisi binafsi zilizojihusisha na na utoaji huduma wa bila.

“Hali ya shirika la Bima ni nzuri kwasasa na  tangu mwaka 2009 shuka chini hakuna madai yoyote na kama yapo basi ni wale waliohama maeneo au kushindwa kufika kuchukua madai yao ambapo Meneja huyo aliwataka kufika kwenye shirika hilo ili kuchukua madai yao”Alisema  Mdenye.

Alibainisha kuwa  zaidi ya shilingi billion 935 zimeweza kulipa madai yaliyokuwepo kwa wadai na kubainisha kuwa miaka ya 2009 kurudi nyuma madai hayo  yalichangiwa na shirika kukabiliwa na changamoto ya kuwepo kwa maradhi mengi ikiwemo UKIMWI ambayo yalichangia kuwepo kwa vifo vingi.

Kwa upande wa mawakala wanaojishughulisha na masuala ya bima ambao wamekuwa wakisababisha usumbufu mkubwa kwa wateja alisema mawakala hao wanawajibu wa kuwaelimisha wateja umuhimu wa kujiunga pamoja na huduma mbalimbali za bima,lakini kama watakuwa wanafanya kinyume wakibainika watachukua hatua za kisheria.

No comments:

Post a Comment