Sunday, April 1, 2012

KADA NA VIONGOZI WA CCM WANENA USHINDI WA CHADEMA ARUMERU.
Nape Mnauye kupitia ukurasa wake wa facebook anasema Hongereni watani (Chadema) kwa ushindi Arumeru Mashariki. Ninawapongeza mmeshinda! Ndio kauli ya wana Arumeru Mashariki nasi tunaiheshimu! Fanyeni kazi kutimiza mliyowaahidi wapiga kura.
anamalizia kwa kusema .Asiyekubali kushindwa siyo ..akaachilia hapo
Ndg zangu Kwanza Nitumie nafasi Hii Binafsi kuwapongeza Chadema kwa Ushindi Wa Arumeru Mashariki,Kiwira,Kirumba,Liziboni na Pia Cuf kwa Ushindi Wa Kata ya Tanga

Nimeamua kufanya hivi kwa Misingi ya kidemokrasia ni wapongeze mmepewa heshima hiyo watumikieni

Ninawapongeza Pia kwakua uchaguzi huu Kama Viongozi Wa CHAMA changu Watatumia Busara basi hili nifunzo kubwa na Nina washaukuru CDM Matokeo haya kutupa Ishara kuwa Kaskazini inaanza kupotea mikononi Kwetu,Kusini Nyanda za Juu inaanza kupotea,Kanda ya Ziwa inaanza kupotea hii ni Alarm kwa CHAMA changu umewadia wakati kwa ujumbe huu Viongozi wakuu warudi ktk Round Table kujadili upya na kutazama Kama makundi yetu yakaisaidia CHAMA

Kwa Matokeo haya Kanda ya Ziwa Alikuwepo Samwel Sitta,Kwa Maana ya KIRUMBA,Mbeya Alikuwepo Mama Anne Kilango,kwa Maana ya Kiwira, Arumeru Alikuwepo Mzee MKAPA,Mzee Mkama,Mzee Lowasa,Ndg yangu Nape ,Liziboni Dk Nchimbi na maaneo haya yote Tumeshindwa umewadia wakati Wa KUJITAFAKARI na kujiangalia kwa kina na si kuja na majibu Kama Yale tuliokuja nayo Baada ya Uchaguzi Mkuu 2010,Tunatakiwa kuja na MAJAWABU

Ninadhani demeokrasia imeheshimika na CCM tumekua tukisahau wajibu wetu Wa kujadili matatizo ya watu toka mwaka 2007 Mpaka sasa 2012 ,wananchi walitupa 1st Workup call 2010 hatukuamka and this is a 2nd Workup Call hatuna Budi kuwashukuru wananchi bcs Wametupa 2nd chance ya kuamka Tujitafakari UPYA

Nimelizie kuwwapongeza CUF na CDM kwa Ushindi wao niwatakie kila la kheri Asanteni kwa kutuamsha Mara ya Pili
                                                                               

No comments:

Post a Comment