Saturday, March 31, 2012

Jeshi la Polisi Nchini limeanzisha utaratibu mpya wa kuwafanyia askari wake tathimini 

 IGP Saidi Mwema akitoa hotuba yake wakati wa kufunga mafunzo hayo.

Mgeni Rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil

Makachero wapya hao.. 

Jeshi la Polisi Nchini limeanzisha utaratibu mpya wa kuwafanyia askari wake tathimini kila baada ya miaka mitatu kwa ajili ya kuboresha utendaji wa jeshi hilo.

Hayo yalizungumzwa jana na Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Saidi Mwema wakati wa kufunga mafunzo kwa askari polisi kwenye chuo cha taaluma cha (CCP)kilichopo Mjini Moshi.

Alisema kuwa tathmini hiyo itatoa nafasi kwa askari polisi ambao watakuwa wanafanya vizuri kuendelea na utandaji ndani ya Jeshi hilo,lakini kwa wale ambao watakuwa hawafanyi vizuri Jeshi hilo litasitisha mkataba wa kuendelea kuwa mtumishi.

Mwema alisema Jeshi hilo limeamua kufanya hivyo ili kuweza kuwatumikia wananchi waliowaajiri kwa uadilifu,pamoja an kuondoa malalamiko ambayo yamekuwepo kwa baadhi ya askari.

Hata hivyo alisema tathmini hiyo,haitawahurumia askari ambao hawatakuwa na sifa,na watanyimwa mikataba ya kuendelea na utumishi,hivyo kutakuwa kwenda kufanya kazi nyingine uraiani.

“Kwa viongozi wa juu wakiwemo Makamanda katika Komandi yoyote,wanatakiwa kuwa waadilifu na kama wataona askari yoyote utendaji wake hauridhishi atoe taairfa kwenye ngazi za juu kwa miezi mitatu ili askari aweze kutoa sababu alisema Mwema.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi ambaye alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil alisema licha ya kuwepo kwa mafanikio kwa jeshi hilo ila bado hayajasaidia kupunguza matukio yanayoendelea kulichafua jeshi hilo.

Miongoni mwa matukio ambayo yaliyotajwa na Katibu huyo kwa jeshi la polisi ni pamoja an kuendekea kuwepo kwa matukio kwa askari  kujihusisha na rushwa na kuwabambikia wananchi keshi na kuwatesa raia,vitendo vya utovu wa nidhamu mitaani,ambavyo vinaendelea kuchafua jeshi hilo.

Alisema kuwa kwa Polisi ambao wamekuwa na tabia za utovu wa nidhamu wanatakiwa kuondolewa ili kuendelea kulinda heshima ya jeshi hilo.

Katika mahafali hayo wanafunzi waliofanya mtihani 3264 waliofaulu mtihani walikuwa 3210 na waliofeli ni 54 walipata nafasi ya kufanya mitihani mwingine,na wakifaulu wataingizwa kazini na ambao watashindwa wataenda kutafuta ajira nyingine.


 

No comments:

Post a Comment