Thursday, March 22, 2012

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI ZUIO LA KUAPISHWA KWA MANGI WA MARANGU FRANK MAREALLE.
KUTOKA KULIA NI WAKILI WA UPANDE WA UTETEZI ALBERT MSANDO ,KATIKA NI MANGI WA MARANGU FRANK MAREALLE,NA KAKA YAKE NA MANGI WILFRED MAREALLE WA MWISHO KUSHITI WAKIWA NJE YA MAHAKAMA BAADA YA ZUIO LILILOKUWA LIMEWEKWA MAHAKAMANI KUPINGA KUSIMIKWA KWA MANGI KUTUPILIWA MBALI.
MANGI WA MARANGU FREANK MAREALLE ALIYEVALIA KOFIA YA ASILI,AKIPENA MKONO NA KAKA YAKE AMBAYE NI MWENYEKITI WA UKOO WA MAREALLE WILFRED MAREALLE BAADA KUMALIZIKA KWA KUSIKILIZWA KWA ZUIO LILOKUWEPO MAHKAMANI HAPO.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Manispa ya Moshi imetupilia mbali zuio lililokuwa limefunguliwa mahakamani hapo,la kuzuiwa kusimikwa kwa mangi wa Marangu Frank Marealle,pamoja na zuio la kula chakula cha mchana na wana marangu.

Zuio hilo lilikuwa limefunguliwa mahakamani hapo na Anita Augustine Marealle,na Willuum Marealle,wakizuiwa kuapishwa kwa Frank Marealle kuwa Mangi wa Marangu.

Akisoma maamuzi  hayo mahakamani hapo Munga Sabuni ambaye ni hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi amesema kuwa hakuna,kesi ya kujibu kututokana na walaliamikaji kuwasilisha maombi ya zuio bila kufungua kesi.

Sabuni amesema kuwa hadi mahakama kufikia uamuzi wa kutupilia mbali maombi hayo ni kutokana na sheria kutaka kuwepo kwa kesi ya msingi ambayo ingekuwa imefunguliwa na Willium Mareale na Anita Marealle mbali na ombi la zuio.

Kwa upande wa wakili wa upande wa utetezi Albert Msando amesema kuwa,endapo zuio hilo lisingeweza kuendelea kupewa nguvu kutokana na walalamikaji kutofuata sheria, huku akisema kuwa  mahakama isingeweza kuendelea kusikiliza maombi  madogo mahakamani kama hakuna kesi ambayo tayari ilikuwa imefikishwa mahakaman.

 

No comments:

Post a Comment