Sunday, June 3, 2012

MWENYEKITI WA HALMASHARI YA MOSHI AKIRI MADIWANI KUWACHAPA VIBOKO  BAADHI YA WANANCHI WANAOKUNYWA POMBE MUDA WA KAZI.

Naibu Waziri wa tawala za serikali za Mitaa(TAMISEMI)Agrey Mwandry akizungumzia suala la kuwepo kwa sheria ndogo kwa ahili ya kuwadhibiti wananchi wanaokunywa pombe muda wa kazi kwenye kiako cha RCC jana
 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Moris Makoi akiwa kwenye moja ya vikao vya halmashauri hiyo.  

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro Moris Makoi amekiri madiwani wa Halmashauri hiyo kuwachapa viboko baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakinywa pombe muda wa kazi kitendo ambacho kilielezwa na Mkuu wa Mkoa kuwa ni kinyume na sheria za nchi kwa viongozi kujichukulia sheria mikononi.

Mwenyekiti huyo wa Halmashauri aliyazungumza suala hilo jana kwenye kikao cha ushauri Mkoa RCC wakati wajumbe mbalimbali wa mkutano huo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama kutaka kujua Wilaya ambayo inaongoza kwa utengenezaji na unywaji wa pombe za kienyeji.

Baada ya kupewa nafasi kwa Mwenyekiti huyo kueleza hali ya Halmashauri ya Moshi alisema kuwa tatizo la unywaji wa pombe kiholela limepungua,baada ya madiwani wa maeneo husika kupambana kwa kuwachapa viboko wananchi ambao wamekuwa wakinywa pombe hizo muda wakazi.

“Nikweli tatizo hilo lipo lakini siyo kubwa kama linavyozungumzwa kutokana na jitihada za madiwani wa maeneo ambalo hilo tatizo limekuwepo wamekuwa wakijitahidi kuwachapa viboko watu ambao wamekuwa ni sugu katika unywaji wa pombe”Alisema Mwenyekiti huyo.

Hata hivyo baada ya Mkuu wa Mkoa kupata maelezo hayo kutoka kwa Mwenyekiti huyo hakuridhishwa na kukemea na kutaka kama wapo madiwani ambao wamekuwa wakifanya hivyo kuacha mara moja la sivyo nao watachukuliwa hatua.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mkuu wa Mkoa Gama alisema kuwa Nchi ambayo inafuata utawala wa sheria haipaswi kuchukua sheria mkononi bali suala hilo linatakiwa kufikishwa kwenye vyombo vya dola na kama watashindwa kulisimamia ipasavyo nao watatakiwa kujieleza.

“Japo tunasimamia mazingira lakini hatupaswi kujichukulia sheria mikononi,tuviachie vyombo vyetu vya dola na hata kama polisi wana madhaifu tuwaseme hii ni nchi inayoongozwa kwa utawala

No comments:

Post a Comment