Thursday, May 3, 2012

NAIBU SPIKA ATAKA VYOMBO VYA HABARI VISIWAONEE HURUMA VIONGOZI MAFISADI

 

NAIBU spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndungai amepongeza kazi nzuri inayofanywa na vyombo vya habari nchini katika kuwafichua viongozi wanaotuhumiwa kwa  Vitendo vya ufisadi huku akitaka vyombo hivyo vya habari kuacha kuwaonea huruma wale wote wanaojiandaa kuja kuwa viongozi wa nchi ambao wanatuhumiwa kwa ufisadi.

Ndungai ambaye ndie alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya kitaifa ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani alitoa  kauli hiyo Leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini D'salaam wakati akiwahutubia wanahabari katika Sherehe zilzoandaliwa na Misa Tanzania na mfuko wa vyombo vya habari Tanzania ( TMF) .


Alisema kuwa wakati wanahabari nchini wanaadhimisha siku ya Uhuru wa vyombo vya habari ni vema wanahabari kuendelea kutathimini mwenendo mzima wa uwajibikaji katika kuandika habari za wale wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

Kwani alisema kuwa pamoja na jitihada mbali mbali vinazofanywa na vyombo vya habari katika kuandika habari za kifisadi ila bado nguvu kubwa inatumika kuwafichua viongozi mafisadi waliopo madarakani na kuwaonea huruma viongozi wajao jambo ambalo ni hatari zaidi .

Alisema kinachotokea leo kwa vyombo vya habari kuandika habari za mafisadi wa sasa waliopo madarakani na kuwaonea huruma viongozi wajao bila kuwasema ni kutolitendea haki Taifa na siku watakaoingia madarakani nchi itayumba zaidi.

Hata hivyo alisema kuwa juhudi za wanahabari na vyombo vya habari nchini katika kuhabarisha umma zimeendelea kuwa kubwa zaidi na kuwa hata shughuli za bunge zimekuwa zikiwafikia wananchi kutokana na ushirikiano mzuri uliopo Kati ya bunge na wanahabari.

"kweli uwajibikaji wa vyombo vya habari kwa sasa ndio umepelekea hata kasi ya wananchi kufuatilia vikao vya bunge kuongezeka zaidi na hata wabunge kuchangia bungeni kuongezeka japo wanahabari mmekuwa mkituchapa sana ....Kwani mara kwa mara mmekuwa mkipiga picha wabunge wanaosinzia japo sisi wabunge hatusemi Kusinzia tunakuwa tunatafakari ......ila nasema kazi nzuri sana mmekuwa mkiifanya" alisema Ndungai 

Katika hatua nyingine naibu spika huyo aliahidi kuwa bunge litaendelea  na ushirikiano na vyombo vya habari na kuwa hata miswaada miwili  itakayofikishwa bungeni juu ya mapendekezo ya Uhuru wa vyombo via habari Pindi itakavyofikishwa bungeni 

No comments:

Post a Comment