Chama cha waandishi wa habari Mkoani Kilimanjaro(MECKI)kimeadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari kwa kujitolea kwenye shughuli za kijamii.
Watoto wanaolelewa na kituo cha treasures of afrika childrens home wakiwasikiliza waandishi wa habari hawapo pichani |
WAANDISHI WA HABARI NA WANACHAMA WA PRESS CLUB YA KILIMANJARO WAKIWASIKILIZA MKURUGENZI MSAIDIZI WA KITUO CHA treasures of afrika childrens homE(hayupo pichani ) |
Picha ya pamoja kati ya waandishi,watoto wanaoishi kwenye kituo cha treasures of afrika childrens home |
Hapa ni Mwandishi wa habari wa gazeti la Habari Leo Arnold swai akipanda mti wake kama sehemu ya kuazimisha siku ya vyombo vya habari. |
Chama cha waandishi wa habari Mkoani
Kilimanjaro(MECKI)kimeeadhimisha siku ya uhuru wa habari kwa kujitolea kwenye
shughuli za kijamii ikiwemo kutoa msaada wa vyakula,vinywaji mafuta na sabuni
kwa kituo cha watoto yatima cha
treasures of afrika childrens
home pamoja na kupanda miti katika
manispaa ya moshi.
Akizungunza wakati wa ziara hiyo Kaimu katibu Mkuu wa
Chama cha waandishi Mkoani hapa Nakajumo James amesema kuwa chama hicho
kimeamua kufanya hivyo kama njia pekee ya
kuwafanya watoto hao wanaoishi kwenye kituo hicho wasione wametengwa na jamii.
Amesema kuwa waandishi wamekuwa wakiandika habari za watu
na taasisi mbalimbali ambao wamekuwa wakijitoa kwenye shughuli hizo,hivyo ni
vyema wakaitumia siku ya vyombo vya habari dunia nao kusaidia watoto yatima
pamoja na watu walio na mahitaji maalumu.
Akizungunmza kwa niaba ya Makamu Mwenyekiti wa Mecki
Mtunza hazina wa chama hicho Jane Mhalila amegusia malezi wanayopatiwa watoto
kuwa ni mazuri na yanaendana na wakati kwa kuzingatia hali halisi ya madaliko
ya kisayansi na teknolojia,na kupata huduma ya kiroho.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa kituo hicho bw Elisonguo
Benjamen Kiwelu amesema kuwa kituo hicho kina watoto wapatao 26 wanaosoma shule
za msingi na sekondari ambao wanakuwa tayari wamedhibitishwa na ustawi wa jamii
kuwa hawana msaada wowote.
Hata hivyo ameseme akuwa kituo hicho kinakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo kupanda kwa garama za maisha,unaotokana na
mfumuko wa bei ya vitu wanavyohitaji wattoo hao.
Kituo cha Treasures
of Afrikan Children home kilianzishwa mwaka 2006 na kuanza kuchukua
motto wa kwanza mwaka 2007 na hadi sasa kina watto wapatao 26 na wafanyakazi
waangalizi 20.
No comments:
Post a Comment