Thursday, October 18, 2012

  KANISA LINGINE LACHIMWA MTO DAR

 
Kuna habari  zisizo rasmi  zimelifikia dawati letu la habari kuhusu uvamizi wa Kanisa moja maeneo ya Yombo- Dar es salaam leo. Inasemekana kuna kundi moja la watu wanaohisiwa kuwa Waumini wa dini ya Kiislam wamelivamia Kanisa ya KKKT  - Yombo, Chingaone Blog imefanikishwa  kuwasiliana na mmoja wa Waumini wa Kanisa hilo aliyekuwepo eneo la tukio, Muumini huyo alikiri kutokea kwa tukio hilo ila alisema watu hao hawakufanikisha zoezi hilo na hii ilitokana na  upinzani  mkali walioupata toka kwa walinzi wawili wa kanisa, ambao mmoja  wao aliamua aligonga kengele  na kusababisha  mkusanyiko wa  watu  na watu hao kufanikiwa kukimbia , hadi sasa hakuna  hata mmoja aliyekamatwa kutokana na tukio hilo...
Endelea kuungana nasi kwa habari zaidi ..........
SOURCE chingaoneblog.

No comments:

Post a Comment