Friday, May 4, 2012

MANISPAA YA MOSHI YAPITISHA BAJETI YA SH BILLION 25.5 KWA MWAKA 2012/2013Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi Bernadetter Kinabo akizungumza kwenye kikao cha bajeti,kushoto ni Meya wa Manispaa ya Moshi Japhary Michael.

                                                    Kikao kinaendelea


Diwani wa Njoro Jomba Khoi akichangia akiwalalamikia watumishi kukaa ofisini na kushjindwa kuwatembelea wananchi kujua kero zao..

Mtumishi ambaye ni Mwekahazina wa Manispaa ya Moshi akifafanua jambo..


Diwani wa Kata ya Longu B Reymond Mboya akichangia hoja kwenye kika cha bajeti..
                                                                          
Kikao cha baraza la Madiwani Manispaa ya Moshi kimepitisha bajeti ya zaidi ya shilingi billion 25.5 ikiwa ni bajeti ya mwaka 2012/2013 kwa ajili ya utekeleza wa shughuli mbalimbali huku kipaumbele kikiwa ni kuboresha huduma za kijamii.

Akizungumza kwenye kikao hicho cha bajeti Mkugenzi wa Manispaa ya Moshi Bernadetter Kinabo alisema kuwa ajeti hiyo imeongezeka kutoka shilingi billion 22 kwa mwaka 2011/12 hadi kufikia billion 25.5 kwa bajeti hii kutokana na ongezeko la mishahara kwa watumishi.

Alisema kwenye bajeti hiyo iliyopitishwa shillingi billion 15 zitatumika kwa ajili ya mishahara ya watumishi,shillingi billion 4 zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo kama uboreshaji wa afya elimu ya msingi na sekondari,pamoja miundombinu.

Hata hivyo katika mapato ya vyanzo vya ndani Kinabo alisema kuwa halmashauri inakadiria kukusanya zaidi ya shilingi billion 4 kwenye bajeti hii kukiwa na nyongeza ya shillingi billion 2 kwa bajeti iliyopita ya mwaka  2011/2012.

Alisema kuwa katika Makusanyo ya mapato halmashauri halmashauri  imeweka nguvu katika mapato yake ya ndani,kwa kushirikiana na madiwani ambapo wameweza kufanikiwa kubuni vyanzo vya ndani ili kutekeleza shuguli mbalimbali za maendeleo.

Katika kusaidia huduma za kijamii bajeti hiyo imetenga shillingi million 200 katika kuangalia watoto yatima  na wanaishi katika mai iozingira magumu ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira mashuleni ikiwemo uboreshaji wa vyoo.

”Kipaumbele ch bajeti ni katika kuboresha huduma za wananchi nao waweze  kukuza uchumi wao ikiwemo ili wananchi waweza kushiriki vyema katika kazi za maendeleo”Alisema Kinabo.

Madiwani mbalimbali wakizungumza na mtandao huu wa www.tanzani-leo.blogspor t.com baada ya kumalizika kwa kikao hicho diwani wa Njoro Jomba Khoi alisema kuwa bajeti hiyo imekizi vigezo na kuwajali wananchi kutokana na kuweka vipaumbelea katika huduma za kijamii.


No comments:

Post a Comment