Diwani wa Kata ya Hai Mjini Japhary Kiure naye aanza harakati za upandaji wa miti.
Diwani wa Kata ya Hai Mjini(kulia)Japhary Michael akipanda mti katika eneo la kingereka lililopo wilayani Hai |
Wakina mama nao hawakuwa nyuma kwenye zoezi hilo. |
Diwani wa Kata ya Hai Mjini (Chadema)Japhary Kiure leo
amepanda miti zaidi ya 100 kwenye mlima wa kingereka uliopo kwenye kata hiyo
Wilayani Hai kwa lengo la kuendeleza harakati za upandaji wa miti na kuboresha
mazingira.
Akizungumza wakati
wa kupanda miti hiyo Bw Kiure amesema kuwa mkakati aliojiwekea baada ya
kuzindua upandaji huo wa miti leo ni kupanda miti maeneo mbalimbali ikiwemo
milima,vyanzo vya maji na maeneo ya makazi ya watu.
Amesema kuwa zoezi hilo la upandaji wa miti amelifanya
kuitikia wito wa kitaifa wa upandaji wa ambapo katika eneo aliliopanda miti la
mlima wa kingereka ulikuwa tayari umekwishaanza kuadhiriwa na mmonyoko wa
udongo kutokana na kukosa miti na kuharibiwa na mifugo.
Kiure amesema kuwa katika kuweka mikakati ya kufanikiwa
kwenye zoezi hilo amekwisha hamasisha waannchi
kupitia kwenye vikao mbalimbali na kutaka kila kaya kupanda miti zaidi ya kumi
pamoja na kujitolea miti kwenye taasisi kama mashule.
Amesem kuwa baada ya kupanda miti 100 aliyoipanda kama uzinduzi,matarajio yake ni kupanda miti zaidi ya
5000 katika kipindi chake cha uongozi ambayo atahakikisha inasimamiwa na
kutunzwa ili isikauke na kuweka utaratibu mzuri wa kudhibiti mifugo ambayo
imekuwa ikiharibu miti hiyo.
Kwa upande awake Abibu adam lema ambaye ni Mwenyekiti wa
Mtaa wa Kingereka amewataka wafugaji kuwa walinzi wa miti ambayo imekuwa
ikipwandwa kwa ajili ya utunzaji wa mazingira,huku akitaka jamii kuwa walinzi
na kuitunza miti ambayo itakwua inapandwa katika maeneo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment