Mchoraji wa Vib
Raia wanne
wa Sweden wamepandishwa kizimbani Denmark ili kujibu mashtaka ya kupanga
shambulio katika ofisi za gazeti moja la Denmark ambalo mwaka 2005 lilichapisha
vibonzo vya kumkashifu Mtume Mohammed.
Jengo la gazeti hilo
liitwalo Jylands Posten liko mjini Copenhagen, nchini Denmark. Kwa sasa jengo
hilo lina vyombo vya usalama vya kila aina pamoja na walinzi ambao kazi yao ni
kuwazuia watu wasio na kibali kuingia katika jengo hilo. Gazeti la Jylands Posten
lina maadui wengi, kwani mwishoni mwa mwaka 2005 gazeti hilo lilichapisha
vibonzo 12 vilivyomwonyesha Mtume Mohammed. Vibonzo hivyo vilizua wimbi la
hasira miongoni mwa waumini wa dini ya kiislamu. Katika nchi nyingi zenye
utawala wa kiislamu, yalifanyika maandamano yaliyoambatana na vurugu ambapo
watu wapatao 150 waliuwawa.
Hasira
za waislamu wenye itikadi kali zimekuwa zikielekezwa kwa gazeti la Jylands
Posten pamoja na mchoraji wa katuni aitwaye Kurt Westergaard, ambaye alichora
katuni ya Mtume Mohammed akiwa amevaa kilemba chenye umbo la bomu. Mara kwa
mara wafanyakazi wa gazeti hilo pamoja na mchoraji Westergaard walitishiwa
kuuwawa au kulipuliwa wakiwa ofisini kwao.
Mashtaka yote
yamekanushwa
Miongoni mwa watu
wanaoshukiwa kupanga shambulizi la kigaidi katika ofisi za gazeti hilo ni raia
wanne wa Sweden ambao ni Munir Awad, Omar Abdalla Aboelazm, Munir Ben Mohammed
Dhahri na Sabhi Ben Mohammed Zalouti. Washukiwa hao walikamatwa na polisi mwaka
2010 baada ya mashirika ya ujasusi ya Denmark na Sweden kuwafuatilia kwa miezi
kadhaa. Mbali na kushtakiwa kwa kosa la ugaidi, watu hao watajibu pia shtaka la
kubeba silaha bila kibali.
Mchoraji wa vibonzo Kurt
Westergaard
Iwapo watapatikana na
hatia, washukiwa hao wanaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 16. Waendesha
mashtaka wameeleza kwamba wataiomba serikali ya Denmark iwafukuze watu hao
watakapokuwa wamemaliza kifungo chao. Hata hivyo washtakiwa wote wanne
wamekanusha mashtaka hayo.
Hii ni mara ya pili
kuwepo kwa kesi ya namna hiyo, inayohusisha wachoraji wa katuni. Mwaka 2011,
makahama moja ya Denmark ilimhukumu raia mmoja wa nchi hiyo mwenye asili ya
kisomali kwa kosa la ugaidi kwa sababu aliingia katika nyumba ya mchoraji mmoja
wa vibonzo aliyekuwa amechora katuni za Mtume Mohammed. Msomali huyo alimtishia
mchoraji kwa shoka lakini mchoraji huyo alifanikiwa kujifungia katika chumba
kimoja. Mahakama ilimhukumu Msomali huyo kifungo cha miaka 9 jela.
Habari kwa hisabiu ya Dw.
|
No comments:
Post a Comment