RAISI KIKWETE AANZA ZIARA YA SIKU TANO BRAZIL.
![]() |
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Bw Raymond Mbilinyi, baada ya
kuwasili Jumapili Aprili 15, 2012 katika hoteli ya Tivoli
jijini Sao Paulo, Brazil, tayari kwa ziara ya siku
tano ya kikazi nchini humo(picha na habari na Ikulu)
Rais
Jakaya Mrisho kikwete amewasili Brazil Jumapili Aprili 15, 2012 kwa ajili ya
ziara ya kikazi ya siku tano.
Katika
ziara hiyo Rais Kikwete anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji
wake Rais Dilma Varna Rousseff wa Brazil na Rais mstasafu wa nchi hiyo
Mheshimiwa Inacio da Silva Lula na viongozi waandamizi wa nchi hiyo.
Katika
ziara hiyo, Rais Kikwete atahudhuria mkutano wa mwaka wa wakuu wa nchi
zinazoshiriki katika Mpango wa Ubia wa Uwazi Serikalini (Open Government
Partnership-OGP) utakaofanyika mjini Brasilia chini ya Uenyekiti wa Rais
Rousseff na kuhudhuriwa na wajumbe wapatao mia nne (400) kutoka serikalini,
Asasi zisizo za kiserikali, Sekta binafsi pamoja na Mashirika ya Kimataifa.
Ubia wa
Uwazi Serikalini au kwa kifupi OGP, ni mpango uliozinduliwa Septemba 2011 mjini
New York, Marekani kwa lengo la kuwapa wananchi nafasi ya kushiriki katika
kuamua mambo yanayowahusu, kupitia vyama visivyo vya Kiserikali na vya Kijamii.
Ubia huu
unashirikisha kwa usawa wawakilishi wa serikali kwa upande mmoja na wawakilishi
wa Asasi zisizo za Kiserikali za Kijamii kwa upande mwingine. Nchi ya Brazil
kwa kushirikiana na Marekani imekuwa mstari wa mbele katika kusukuma ubia huu.
Rais
Kikwete anatarajiwa kuhutubia mkutano huo tarehe 17 Aprili, asubuhi mara tu
baada ya hotuba ya ufunguzi itakayotolewa na Mwenyekiti wa mkutano huo Rais
Dilma Rousseff wa Brazil, ambapo ataelezea maendeleo iliyofikia katika kuandaa
mpango kazi wa kutekeleza ahadi ya kuongeza uwazi kama ilivyokubaliwa katika
kikao kilichofanyika Disemba 2011.
Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nchini tarehe 20 Aprili, 2012.
Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nchini tarehe 20 Aprili, 2012.
No comments:
Post a Comment