Sunday, March 11, 2012

WANANCHI WA KIJIJI CHA MIJONGWENI WILAYANI HAI WALILIA UPATIKANAJI WA DARAJA LA KUDUMU..pichani ni mkazi wa kijiji cha mijongweni akivuka kwenye daraja la mnepo linalotumia hivi sasa.

Kama inavyoonekana pichani ni kivuko cha mnepo ambacho kinatumiwa na wananchi wa kijiji cha Mijongweni kilichopo Hai Mkoani Kilimanjaro.

Mmiliki wa blog hii alitembelea hadi eneo hilo na kusikiliza kilio cha wananchi hao,ambao walisema kuwa kwa mwezi wanaopoteza maisha ni wananchi hadi wanne wanaodondoka kutokana na daraja hilo.


Kwa mujibu wa kumbukumbu zangu,kiako cha ushauri kilichokaa january mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama,aliutaka uongozi wa Halmashari ya Wialya ya Hai kuhakikisha kuwa unafanya jitihada za makusudi kulifanyia maboresho daraja hilo.

ili  kuondoa adha ambayo wananchi wamekuwa wakikumbana nayo.

Wanachoofia wananchi hao ni Mvua ambazo zimeanza kunyesha na ambazo zitanyesha msimu huu wa masika,kwani wapo wanafunzi ambao wanatoka kijiji cha mijongweni na kwenda kwenye vijiji vya kikavu chini kufuata huduma mbalimbali ikiwemo shule.

Lakini wanasema hali ni tofauti wakati wa masika kwani hulazimu wakina mama ambao wanakuwa na mizigo kuwalipa vijana 500 hadi 1000 kuvusha mzigo wenye kilo 50 na kuendelea.

wananchi wanasema kuwa daraja hilo la mnepo hivi sasa limekuwa chakavu,na kusema wananchi wapoteza maisha kwa wingi ni wazee na  wakina mama na watoto,hususani nyakati za masika.
Imewekwa na Rodrick Mushi wa Blog ya tanzania-leo.blogsport.com

No comments:

Post a Comment