……………………………………………………….
Ndugu Wanahabari,
Nimelazimika nizungumze nanyi
kuhusu tukio la kuuwawa kwa Padre Evaristi Mushi wa Kanisa Katoliki
Zanzibar lililotokea leo asubuhi tarehe 17 Februari, 2013 eneo la Mtoni
mkoa wa Mjini Magharibi, ambapo watu wasiofahamika walimpiga risasi
Padre huyo alipokuwa anaenda kusalisha ibada katika kanisa la Betras.
Baada ya tukio hilo kutokea alikimbizwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja,
ambapo baadae alifariki dunia. Tukio hili ni baya na la kusikitisha.
2 Kufuatia kutokea kwa tukio hilo
na kujirudiarudia kwa vitendo vya kuwashambulia na kuwadhuru viongozi
wa dini na uchomaji wa nyumba za ibada, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana
na vyombo vingine vya ulinzi na usalama tumeanza uchunguzi wa kina wa
kuwatafuta wanaohusika na matukio hayo.
3Hivyo, nimetuma timu ya wataalam
waliobobea kwenye masuala ya upelelezi na oparesheni kutoka Makao Makuu
ya Polisi, kwenda kushirikiana na timu ya wataalam iliyoko Zanzibar.
Hadi sasa watu watatu wananshikiliwa kwa mahojiano.
Jeshi la Polisi limeimarisha
doria maeneo yote hapa nchini na tunafuatilia mienendo na kuakamata watu
wote wanaochochea, kufadhili, kuhamasisha na kushiriki katika vitendo
vya uhalifu, vurugu na fujo.
Tukiwa katika kipindi hiki,
nawaomba wananchi wote hapa nchini kuwa watulivu wakati suala hili
linaposhughulikiwa kuhakikisha kwamba wahalifu hao wanakamatwa na sheria
inachukua mkondo wake.
Naomba nitumie fursa hii pia,
kuwasiliana na wananchi wenzangu wenye taarifa zitakazosaidia wahalifu
hao kukamatwa kutupa ushirikiano kupitia namba zetu maalum za simu
zifuatazo 0754785557 au 0782417247 na namba za makamanda wa mikoa na
vikosi, ili kuhakikisha kwamba amani, usalama na utulivu vinadumishwa
hapa nchini.
Nawashukuru wananchi wote ambao wamekuwa wakitupa ushirikiano.
No comments:
Post a Comment