Friday, April 6, 2012

RC KILIMANJARO AVIKALIA KOONI VIWANDA VINAVYOTUMIA MAGOGO KILIMANJARO.
 

                                                      RC KILIMANJARO LEONIDAS GAMA.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama amepiga marufuku viwanda vyote vinavyotumia magogo mkoani hapa, kutoingia mkataba wa uvunaji miti na watu wasiokuwa na mashamba, na badala yake amevitaka kilima mashamba yao wenyewe ili viweze kujiendesha.

Gama aliyasema hayo jana wakati wa operesheni ya siku kumi ya  kupanda miti 29,000 katika eneo la ukanda wa hafu maili lililopo wilaya ya Moshi vijijini, ambapo alisema kuwa wamiliki wa viwanda vinavyotumia magogo wamekuwa wakiingia mikataba na watu wasikuwa na mashaamba ambao huwapeleka kuvuna miti ya asili kwenye msitu wa mlima Kilimanjaro.

Alisema kuwa viwanda hivyo vinapaswa kulima mashamba yao ya kuvuna magogo na sio kufanya uharibifu kwenye misti ya asili,  hali aliyosema inapelekea mkoa wa Kilimanjaro kuwa jangwa.

Gama alivitaka viwanda hivyo kuingia mikataba kwenye misitu ya serikali nasio kuvuna miti kiholela, na kuzitaka halimashauri zote kusimamia sheria za misitu kikamilifu lengo likiwa ni kurudisha misti yote ya asili inayozunguka milima na barafu yake.

Alisema kuwa kwasasa  ukame uliopo mkoani hapa unatishia uhai wa wananchi, kutokana na mito na chemu Chemu iliyokuwa ikitiririsha maji toka mlimani kukauka sababu zikiwa ni kilimo kandokando ya vyanzo vya maji, ukataji miti ovyo pamoja na uchomaji mioto.

Gama alisema kuwa lazima kila halimashauri iwajibike kuhakikisha inasimamia sheria za misitu, ikiwa ni pamoja na kudhibiti mifugo ambayo  faini yake alisistiza iwe kubwa kuliko bei ya mfugo wenyewe, pamoja na kutoa zawadi kwa mtu atakaetoa taarifa za mashine ya kuvuna miti “chensoo”.

Tunanata tufikie lengo la kerejesha uoto wa awali, hivyo halimashauri zitatoa shilingi 50,000 kwa mtu atakae toa taarifa ya kutumika kwa mashene ya kuangusha miti “Chensoo” pia zitaoa shilingi 50,000 kwa mtu atakaeonyesha sehemu mti ulipokatwa siku hiyo na kudhibitishwa” alisema Gama.

Gama alisema kwa ukanda huo jana walifanikiwa kupanda miti 2,100 ambapo katika eneo hilo lengo ni kupanda miti 29,000 na kueleza kuwa katika operesheni hiyo ya siku kumi lengo ni kuhakikisha wanapanda miti milioni 8.2 kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali, mashule, hosptali na mtu mmoja mmoja.



No comments:

Post a Comment