JESHI LA POLISI LAMFUKUZA ASKARI ALIYEFANYA FUJO PUB ALBERTO KAZI........
Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limemfukuza kazi
askari wake aliyefanya vurugu disko pamoja na kukutwa na misokoto minne ya
bangi.
Akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Absalom Mwakyoma alisema kuwa jeshi hilo limemfukuza rasmi askari huyo baada ya kufikishwa kwenye mahakama ya kijeshi na kukutwa na makosa mawili ya jinai.
Akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Absalom Mwakyoma alisema kuwa jeshi hilo limemfukuza rasmi askari huyo baada ya kufikishwa kwenye mahakama ya kijeshi na kukutwa na makosa mawili ya jinai.
Tukio la askari
aliyefukuzwa kuingua kwenye ukumbi wa starehe na kufanya vurugu lilitokea March
2 mwaka huu baada ya askari huyo ambaye aliingia eneo hilo majira ya saa 6
usiku na kuanza kufanya vurugu pamoja na shambulio kwa mmliki wa Christopher
Shayo pamoja na mlinzi..
Mwakyoma alisema kuwa askari huyo mwenye namba G8415
Deogratiasi Matious (22) alifanya fujo
na kisha kumshambulia mlizi wa ukumbi wa disko wa Pub Alberto Rajabu Mohamedi na kummuumiza kwa kumng’ata
kwenye mkono.
Hata hivyo alisema kuwa kosa lingine alilofanya askari
huyo aliyefukuzwa ni pamoja na kukutwa na misokoto 4 ya bangi ikiwa mfukoni
mwake,hivyo makosa hayo mawili ndio yaliyomfukuzisha kazi.
Alisema kuwa jeshi hilo
limefanya hivyo kutokana na kuwepo kwa malalamiko kwa baadhi ya askari kukiuka
maadili ya jeshi hilo.
Katika wakati mwingine alisema kuwa baada ya kufukuzwa
kazi atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili,na kazi hiyo
imekabidhiwa kwa mwanasheria wa Serikali ili kulifikisha shauri hilo Mahakamani.
Mwakyoma alisema kuwa kwa mwaka 2011/2012 askari wapatao
18 wameshafukuzwa kazi kutokana na utovu wa nidhamu ikiwemo kukiuka maaadili ya
Jeshi hilo.
No comments:
Post a Comment