MWANANCHI AOMBA MSAADA WA KISHERIA BAADA YA KUDHULIMIWA SHAMBA NA WENYE UWEZO WA KIFEDHA.
Mkazi wa Old Moshi ambaye anajishughulisha na kilimo Shedrack
Lyatuu (53) ameiomba Serikali kuingilia kati dhuluma ya kunyanganywa shamba lake lenye
ukubwa wa hekari nne lililopo kijiji cha Sango kwa kuuzwa kwa mfanyabiashara John
Mwase kinyume na makubaliano yake.
Akizungumza na waandishi wa habari Shedraki alisema kuwa
shauri hilo
tayari lilikwishapelekwa mahakamani likiwa shauri namba 56 la mwaka 2011 kwenye
mahakama ya moshi wahusika wakiwa ni Shedrack Lyatuu na Henry Samky.
Shedrack alisema kuwa alikabidhiwa eneo hilo ambalo ni la uridhi febriari 6 mwaka 2007 na kusema kuwa baada ya
kukabidhiwa alifanya shughuli za kilimo mwaka 2010 na wakati akiendelea kulima
ndipo alianza kukuta mambo ya ajabu ambayo yanamahusiano na ushirikikana.
Alisema kuwa mwaka mwaka 2011wakati akijiandaa na kilimo alikuta
mawe yameweka shambani na akaendelea kulima ndipo aliripoti polisi Mhusika
akafika na kusema ameuziwa shamba na Henry Samky.
“Nilifika shamabani kwa ajili ya kilimo walivyonikuta wakanikamata na kunipeleka
polisi mwaka 2011 ilikuwa January,na kesi ikafunguliwa kwa kumzuia kumzuia
mhusika asifanye shughuli za ujenzi kwenye shamba lake licha
ya kwamba mimi nlikuwa sijauza shama langu”Alisema Lyatuu.
Alisema kuwa Henry Samky ambaye ndiye aliyemuuzia Ambrose
Mwase mkataba aliouonesha hakua halali kutokana na kuonesha kuwa alimuuzia
shamba hili mwaka 1990 wakati shamba hilo
alikabidhiwa mwaka 2007.
Hata hivyo alisema kuwa licha ya hukumu ya kesi iliyokuwa
mahakamanu ambayo ilitolewa hukumu mwaka jana mwezi wa 12 hukumu hiyo haiokuwa
ya haki kutoka na Shedrack kuonekana kama yeye
ndiye aliyekuwa analalamikiwa lakini kutokana na kukosa uwezo wa uelewa wa
kisheria amekosa la kufanya.
Mimi nilisafiri kwenda mbeya desemba 1984 na na kurudi nyumbani mwaka 2006 na mwaka
februari 6 mwaka 2007 nikakabidhiwa shamba la uridhi mimi na kaka yangupamoja
na wazee wa mila sasa nashangaa huo mkataba wa kuuza shamba mwaka 1990
nilisaini lini”Alilalamika Shedrack.
Kwa upande wa Mfanyabiashara anayelalamikiwa kununua
shamba hilo John Ambrose Mwase alisema kuwa shamba hilo alinunua kwa Henry
Samky baada kumhakikishia kuwa shamba hilo ni lake na kumuonyesha mkataba
alionunua kwa mmiliki wa shamba hilo ambaye ni Shedrack Lyatuu.
No comments:
Post a Comment