BREAKING......NEWS MWENYEKITI WA UVCCM ARUSHA AHAMIA CHADEMA.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Mkoani Arusha,James Ole Millya anayeonekana pichani.
Kama alivyosikika akiongea Radio 5 iliyopo jijini Arusha Mwenyekiti huyo amesikika akisema kuwa ameamua kukihama chama cha mapinduzi kwa madai kuwa siyo baba au mama yake..
KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI NAPE MNAUYE
AZUNGUMZIA kuhama kwa Millya
kauli yake hii hapa kupitia ukurasa wa facebook
ampongeza
Millya kwa kuamua kukisaidia Chama Changu, kwani alishakuwa mzigo
mkubwa kwa CCM. Itakumbukwa alikuwa afukuzwe kwenye chama kutokana na
mambo alokuwa akifanya. Akapewa KARIPIO ili apate muda wa kurekebisha
tabia yake! Kaondoka akiwa chini ya karipio. Kajivua gamba,tunampongeza
kwa kuitikia wito wa kujivua gamba. Kila lakheri aendako ni kijana bado
anayo mengi ya kujifunza
No comments:
Post a Comment