Tuesday, March 20, 2012

Dk. Slaa, ajibu mapigo ya Wassira kwa Wasira
Asema aliwahi kuhukumiwa kwa ubabe

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Dk.Wilbroad Slaa, amejibu mapigo dhidi ya Mbunge wa Bunda Stephen Wassira, hukuakisema kuwa hana sifa za kuwa kiongozi, kwa kuwa alihukumiwa kwa kesi yakuvunja sheria kibabe na rushwa katika uchaguzi.

Kauli aliitoa jana alipokuwa akihutubia mikutano ya kumnadimgombea Ubunge kupitia CHADEMA Joshua Nassari katika Vijiji vya Migandini,Ambueni na Mbuguni, ambapo alisema Wassira, amekuwa akisema maneno ya uongodhidi ya CHADEMA na viongozi wake hali ya kuwa hana usafi mbele ya jamii.

Dk. Slaa, alisema hivi sasa kampeni hizo Wassira, amekuwaakitumia maneno ya uongo na rushwa ili kuweza kupata kura kwa njia ya hilabadala ya kujenga na hoja na sera kwa mujibu wa sheria.

“Leo nimekuja hapa nina ushahidi wa karatasi dhidi yaWassira, ambaye amekuwa akitumia propaganda na uongo na uropokaji dhidi yanguna chama chetu cha CHADEMA. Kama yeye ni msafi nahitaji aje kujibuushahidi huu.

“Mwaka 1985, ilifunguliwa kesi dhidi ya Hamis Masisi nawenzake sita, ambapo ipo katika kitabu cha rekodi cha Tanganyika Law, naalishtakiwa kwa kosa la kuvunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  na ilifunguliwa na Hamis Masisi na wenzake nakusikilizwa na Jaji Mfalila.

“Wassira, akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, alitumia ubabe nakuamuru Hamis Masisi na wenzake wakamate kutokana na uababe wake ambapo naowalikata rufaa kwa mahakama ya juu.

“Na ilipofika mahakama Rufaa Wassira alihukumiwa kwa kosala kuvunja Katiba na ubabe, na haikuishia hapo hata mwaka 1997 alifunguliwakesi Mahakama Kuu iliyofunguliwa na Joseph Sinde Warioba dhidi ya StevenWassira, ambapo napo mahakama ilimkuta na kosa la kutoa rushwa, kwa hilininashangaa inakuaje mtu kama huyo anasema uongo  na anapewa Uwaziri wa Mahusiano?,” alisema nakuhoji Dk. Slaa.

Alisea kutokana na ukumu hizo ni vema Rais Jakaya Kikwete,amuangalie kwa kina Waziri wake huyo ambaye amekuwa akisema uongo mbele yajamii hali ya kuwa Watanzania na wananchi wa jimbo la Arumeru Masharikiwakihitaji huduma za kijamii hasa za elimu, maji na pembejeo za kiliomo.

Alisema kutokana na hali hiyo hivi sasa Taifa na Maisha yaWatanzania amekuwa yakizidi kuwa magumu kila kukicha kutokana na mfumo mbovu waSerikali pamoja na Chama tawala.

 “Maisha yanakuwamagumu watanzania wanakosa huduma za afya huku mama wajawazito wakisafirishwakwa Punda kwenda katika hospitali kwa ya kujifungua. Uchaguzi huu tumieni hakiyenu ya kuchagua kwa maslahi ya maisha yenu na Watanzania kwa ujumla.

Akzungumzia hatua ya viongozi wa CCM kuwatumia wachungaji,Dk. Slaa, alisema kuwa hatua ya Katibu wa Halmashauri Kuu Fedha na UchumiMwigulu Nchemba, kuvamia mkutano wa wachungaji na kutoa fedha ni kinyume namaadili ya Taifa.

“Najua kuna kila hila za kuwarubuni Wananchi wa ArumeruMashariki, na juzi Nchemba, alivamia mkutano wa Wachungaji wa Kanisa laWalutheli na kutoa mchango wa Sh. milioni 2, tena akimtumia Mbunge wa NkengeAsumpta Mshama eti nae ni Mchungaji.

“Alipobanwa zaidi mbunge huyo ili aeleze uchungaji wake,alishindwa kujibu na kusema kuwa yeye ni Msaidizi wa Mchungaji, hii ni dalilitosha sasa CCM inaelekea mwisho wake,” alisema Dk. Slaa.

Kwa upande wake Mgombea Ubunge kupita CHADEMA Joshua Nassari,aliwaomba wananchi wa Arumeru Mashariki wamchague ili aeze kutekeleza ilani yachama chake pamoja na kutete maslahi ya wapiga kura wake.

“Nanua tuna mambo mengi ya msingi lakini kubwa hatuwezikuona huduma ya maji inapatika katika mashamba ya wawekezaji wakubwa kutokanchi Afrika Kusini na Zimbabwe huku sisi tukiendelea kutaabika. Sasa nimedharianichagueni ili kuweza kusafisha na kuondoa unyanyasaji ndani ya jimbo letu,”alisema Nassari

Na Mwandishi Wetu Arumeru







No comments:

Post a Comment