MWANDISHI TANZANIA DAIMA ANUSURIKA KUUAWA KILIMANJARO.
Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania
Daima Mkoani Kilimanjaro,Charles Ndagula,amenusurika kuuawa baada ya watu
wanaosadikiwa kuwa ni wafanyabiashara wa magendo ya sukari kumgonga na gari na
kuumiza sehemu mbalimbali za mwili.
Akizungumza kwa shida akiwa amelazwa hospitali
ya St Joseph
iliyopo Mjini hapa Ndagula alisema kuwa aligongwa na gari dogo aina ya Toyota
Rava4 yenye namba T 265 AUE.
Ndagula alisema kugongwa kwake kumekuja baada
ya kupata taarifa kwa mtoa taarifa ya kuwepo magari zaidi ya 12 ambayo yalikuwa
yamepakia sukari, tayari kwa ajili ya kwenda Kenya kwa kupitia njia za panya
Wilayani Rombo.
Alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo
akiwa na mwandishi mwenzake wa Mwananchi,Daniel Mjema,walianza kufuatilia
magari hayo kupitia njia ya Holili kuelekea Rombo ikiwa ni majira ya saa 6:00
usiku.
Walipopita eneo la Holili kuelekea Rombo eneo ambalo
linachimbwa udongo wa ‘pozolana’ ambao unatumika kutengenezea sementi ndipo
walipokutana na magari mawili yakiwa na sukari aina ya fuso yenye namba T
288BHF na lingine likiwa na namba T280 BUZ.
Alisema baada ya kuona magari hayo yakiwa na
sukari walimtaarifu kamanda wa Polisi Robert Boaz kumueleza kilichokuwa
kinaendelea.
Wakati wakiwa bado katika eneo la tukio
wakiendelea na kazi,ambapo zaidi ya magari nane yakiwa na sukari yalikuwa
yamekwishapita, ndipo ilifika gari ndo,aina ya Toyota RAV4 yenye namba T265 AUE
na kupaki mbele ya alipokuwa amesimama Ndagula.
Alisema kuwa akiendelea kuandika namba za
magari yaliyokuwa yanapita,ikiwemo pamoja na gari ndogo ambalo linasadikiwa
kuwa mmoja wa wafanyabishara mwenye mzigo huo wa magendo.
“Wakati nikiwa nimesimama mbele ya gari
dogo,ndipo mtu mmoja alitoka kwneye magari mawili yalikuwa yamepaki na kuingia
kwenye gari dogo na kunifuata nilipokuwa na kunigonga na kuanguka”Alisema
Ndagula.
Hata hivyo alisema kuwa kilichosaidia ni
kuliona gari dogo wakati likimfuata kwa makusudi kwa lengo la kumgonga na
kulikwepa lakini likamuumiza sehemu mbalimbali za mwili.
Hata hivyo jitihada za kumtafuta kamanda wa
Polisi Mkoani Kilimanjaro,Robert Boaz kudhitisha tukio hilo zimeshindikana baada ya kupiga simu yake
ya mkononi bila kupatikana.
Swali
la kujiuliza ni kwamba Polisi wetu na
viongozi wa usalama wanafanya kazi gani kama watu wachache kwa maslahi
yao binafsi wanaamua kuvunja
sheria zilizowekwa na hili siyo kwamba wamekuwa hawafahamu la hasha
biashara ya megendo ipo na inaendelea kufanyika kila kukicha.
No comments:
Post a Comment