TGNP YAWANOA WANAHARAKATI TOKA MIKOANI
Washiriki wa mafunzo hayo |
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo yaliyoandaliwa na TGNP
Na Francis Godwin..
Mtandao
wa jinsia Tanzania (TGNP) umezindua warsha ya uraghbishi ya wiki
moja kwa wanaharakati kutoka mikoani pamoja na Dar es Salaam, ili
kunoa uwezo wao wa kufanya kazi na jamii husika kuibua masuala nyeti
katika jamii hizo zikiwemo mafanikio na changamoto, kuchambua
visababishi vya matatizo au mafanikio hayo kwa kina na kupanga mikakati
ya kushughulikia kero hizo pamoja na wanajamii .
Warsha
hiyo inalenga kuimarisha uelewa wa pamoja wa mtizamo ya kiitikadi
kuhusu dhana za ukombozi wa wanawake kimapinduzi na makundi yaliyoko
pembezoni na kuitekeleza kwa vitendo; kujenga uelewa wa pamoja
kuhusu uraghbishi na mbinu shirikishi zinazotumika katika
uraghbishi, kuongeza uelewa wa kampeni ya hiaki ya uchumi katika
kudai kazi zenye heshima utu na kipato, uhifadhi wa kumbukumbu, mbinu za
mawasiliano na uwezo wa kuvitumia katika Ujenzi wa Vuguvugu la
ukombozi wa wanawake kimapinduzi katika ngazi ya kanda.
Wawezeshaji
wa warsha hiyo ni Bw. Richard Mabala Mkurugenzi wa TAMASHA ambayo
ni asasi ya kiraia iliyobobea katika kuwawezesha vijana na jamii kwa
ujumle kutumia mbinu za uraghbishi kama chachu ya kuleta mabadiliko
chanya katika jamii husika. Bw. Winston Chuchil Mkurugenzi Msaidizi wa
TAMASHA ni mwezeshaji mwenza ambaye naye pia amebobea katika mbinu za
uraghbishi.
Washiriki
wa Warsha hiyo wametoka katika mikoa ya Shinyanga, Morogoro, Arusha,
Dodoma, Mwanza , Mbeya, Dar es Salaam na Pwani wakiwakilisha asasi
mbalimbali za kiraia ambazo zimekuwa mstari wa mbele katika kuleta
mabadiliko chanya katika jamii za mikoa husika.
Baada
ya warsha washiriki wakishirikiana wanajamii na TGNP wataendesha
zoezi la uraghbishi katika mikoa husika ambapo watatumia mbinu mbali
mbali za uraghbishi katika kuibua masuala nyeti yanayogusa jamii
husika, kuyachambua kwa kina ili kupata kiini cha matatizo au mafanikio,
hayo na kutafuta mbinu mbali mbali za kutafuta ufumbuzi wa matatizo
hayo, mbinu zitakazotumika, nani atafanya nini kuanzia ngazi binafsi,
jamii na taifa.
No comments:
Post a Comment