Sunday, May 27, 2012


                  WANANCHI WANAOZUNGUKA MLIMA KILIMANJARO WATAKIWA KUUTUNZA MLIMA HUO KWA   KUFANYA USAFI.
 
                                                      
Wananchi  wanaoishi katika Vijiji vinavyouzunguka milima Kilimanjaro, wametakiwa kujijengea tabia ya kufanya usafi  ndani na nje ya mlima huo, kwa lengo la kuokoa Ikolojia ambayo imeonekana kuuadhiri kwa kiasi kikubwa hususani kwenye vyanzo vya maji.
Wito huo ulitolewa jana na Kaimu katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro Gadison  Lengwana wakati wa kuzindua kampeni ya kufanya usafi ndani ya mlima huo, ambapo jumla ya watu 90 walipanda kwaajili ya zoezi hilo.
Lengwana alisemaa kuwa uchafu mwingi umekuwa ukichangiwa na wapagazi na waongoza watalii, kutokana na wao kutupa taka ngumu kandokando ya barabara na kuziacha, hali inayochangia uhariifu mkubwa wa mazingira.
Alisema kuwa kutokana na  taka hizo zinaweza kuhatarisha Ikolojia ya mlimaa, vyanzo vya maji, pamoja na kupunguza  idadi ya wagenia endapo hatua za hara hazitachukuliwa kwa mamlaka husika pamoja na jamii iliyoko karibu na hifadhi ya mlima huo.
Lengwana alisema kuwa elimu inahitajika zaidi kwa watanzania hususani wanaopanda  juu ya umuhimu wa kusafisha na kuhifadhi misitu ya asilihi  kwa kupanda miti mingi kwa lengo la kuendeleza Ikolojia yam lima huo.
Kwa upande wake mhifadhi mkuu wa Mlima Kilimanjaro KINAPA, Erastos Kufungulo, alisema kuwa lengo la kushirikisha jumuia zote zinazouzunguka mlima kuona umuhimu wa kuifadhi na kuboresha mazingira.
Alisema kuwa kampeni hiyo imeshirikisha wafanyakazi wa hifadhi ya mlima huo na baadhi ya  wananchi, ambapo watapanda wakifanya usafi hadi kileleni  kwa siku kumi wakipitia njia tatu za Machame, Marangu na Mweka.
Mwisho

No comments:

Post a Comment