Sunday, May 6, 2012

BONANZA LA WAANDISHI WA HABARI KILIMANJARO LAFANA..
Kikosi cha timu ya waandishi wa habari Mkoani Kilimanjaro ambacho kimewatoa jasho wafanyakazi wa banki ya CRDB tawi la Moshi baada ya kuwacharaza mabao 3-1.

 
 timu ya mpira inayoundwa na wafanyakazi wa banki ya CRDB tawi la Moshi ambao wamefungwa 3-1 na timu wa waandishi wa habari Mkoani Kilimanjaro,
wachezaji wakiwa mzigoni,waliovalia uzi wa kijani ni timu ya waandishi wa habari Mkoani Kilimanajaro na uzi mweusi ni ile ya wafanyakazi wa banki yua CRDB tawi la Moshi.

 Tupo serious na hii mechi leo lazima tuwafunge,ndivyo walivyokuwa wakijisifu timu ya wafanyakaizi wa banki ya CRDB mwishowe kikawatokea puani..
Mchezaji wa timu ya waandishi wa habari Mkoani Killimanjaro ambaye ni mmiliki wa mtandao wa www,tanzania-leo.blogsport.com,Rodrick Mushi akionyesha manjonjo yake kwenye mchezo huo.

Hapa waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mechi hiyo kwa makini huku wakiwa na furaha baada ya timu hiyo kuongoza kwa bao mbili kipindi cha kwanza.
Hapa Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya bonanza hilo ambaye ni Mjumbe wa Kamati tendaji ya chama cha waandishi wa habari Mkoani hapa(Mecki)Dixon Busagaga,akizungunza jambo muda mfupi baada ya kumalizika kwa bonanza hilo
Leo chama cha waandishi wa habari Mkoani Kilimanjaro kimefanya bonanza lake kwa kucheza na timu ya wafannyakazi wa benki ya CRDB ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya vyombo vya habari ambayo iliadhimishwa mei tatu mwaka huu.

Kwenye bonanza hilo ambalo limeweka rekodi ya aina yake na kuvutia washabiki waliofika kulitazama,timu ya chama cha waandishi wa habari Mkoani Kili,manjaro iliweza kuitandika timu ya wafanyakazin wa benki ya CRDB tawi la Moshi bao 3 -1.

Mechi hiyo ambayo ilikuwa na vuta nikuvute kutokana na wachezaji wa pande zote mbili kuonekana kuchoka mapema,lakini ile ya wafanyakazi wa benki ya CRDB walichoka zaidi kutokana na kutokuwa na maandalizi ya kutosha.

Aliyelipatia bao la kwanza timu ya waandishi wa habari Kilimanajro ni Pascal Mwakyoma kwenye kipindi cha kwanza, likifuatiwa na bao la Arnold Swai,hivyo kusababisha timu hizo kwenda mapumziko wakiwa na 2-0.

Kipindi cha pili mambo yalienda vizuri kwa timu ya waandishi baada ya kupachika bao la tatu,lililofungwa na Dixon Busagaga na hatimaye timu ya Crdb Kujipatia bao moja  la kufutia machozi.

Bonanza hilo ambalo lilikuwa limeandaliwa na Club ya wandishi,wachezaji na washiriki wote waliweza kujipingeza baada ya kumalizika kwa mchuano huo na taratibu nyingine kuendelea.

No comments:

Post a Comment