PANGANI YAENDELEA NA UTAFITI WA MAJI CHINI YA
ARDHI.. |
Afisa wa Maji bonde la Pangani,Hamsa Sadiki
Afisa wa Maji Bonde la Pangani amesema
kuwa mpango wa kuendeleza sekta ya maji bado unaendelea kufanyika kwa uchimbaji wa visima kwenye wilaya za hai na Rombo Mkoani
Kilimanjaro kwa maeneo ya tambarare kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa maji.
Akizungumza ofisini kwake na Mwandishi wa Blog hii,Afisa huyo alisema
kuwa mpango huo pia unafanyika kwa ajili ya utafiti wa maji chini ya ardhi,kwenye
wilaya za Hai na Rombo kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi hususani wanaoishi ukanda wa tambarare.
Alisema kuwa
mpaka sasa visima 15 vimeshakamilika kwa upande wa Wilaya ya Hai na vyote vina
maji huku akisema kuwa kwa upande wa wilaya ya Rombo wameshachimba visima 7
huku kimoja ndo kikiwa na maji kutokana na ukanda huo wa tambarare kuwa na
tatizo la maji chini ya ardhi.
Sadiki alisema kuwa kwenye mpango huo wa kuendeleza
sekta ya maji,chini ya component 1 amesema jumla ya visima 30 vinatarajia
kuchimbwa kwenye wilaya hizo ambao utasaidia kuangalia kazi ambazo zinaweza
kutekelezwa na kuwasaidia wananchi.
Imewekwa na Rodrick Mushi wa Blog ya Tanzania Leo
|
Friday, March 16, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment